Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image may contain: 3 people, people sitting and indoorNa Catherine Sungura, W. Afya

UJUMBE wa wawekezaji kutoka nchini Misri umewasili nchini na kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kwa nia ya kujenga viwanda vya dawa za binadamu zikiwemo za majimaji pamoja na zile za antibiotic.

Ujumbe huo ulikutana jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na wawakilishi kutoka wizara Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC).


Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Image may contain: 3 people, people sitting and indoor Ujumbe huo ulisema watazalisha dawa za majimaji yaani “IV Fluids” pamoja na “antiobiotics” za aina mbalimbali ikiwemo "Paracetamol IV” na dawa za kutibu Malaria.

Ulisisitiza lengo lao ni kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki na ya kati.
 

Katika mazungumzo hayo,wawekezaji hao pia wanatarajia kusaidia Tanzania katika uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatics B na C ).

Waziri Ummy amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo na kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha jambo hilo katika muda uliopangwa.


Image may contain: 9 people, people standing and suit “Naelekeza kwa taasisi zote zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali ya juu ili lengo hili lifikiwe, soko la dawa hapa nchini lipo naomba niwahakikishie hili,”alisema waziri Ummy.

Waziri Ummy aliwaomba wawekezaji hao kuharakisha ujenzi huo ndani ya miezi kumi na nane kama walivyoahidi ili watanzania waanze kunufaika mapema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement