Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image may contain: 1 person, sittingNa  Catherine Sungura, W. Afya - Dodoma

SERIKALI haitosita kumchukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya Umma nchini atakayebainika kuwatoza fedha wananchi katika kutoa huduma ya vipimo vya malaria na au kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.
 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria Duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote.
 http://scd.sw.rfi.fr/sites/kiswahili.filesrfi/imagecache/rfi_16x9_1024_578/sites/images.rfi.fr/files/aef_image/153344519_0.jpg
Jamii ya mbu aambukizae ugonjwa wa Malaria.

Amesisitiza wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.

“Huduma ya kupima Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka kutekeleza agizo hili," amesisitiza.

Amewaagiza waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa karibu ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.
 Waziri Ummy  amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.

Siku ya Malaria Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni “ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement