Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema kwa sasa taasisi hiyo inategemewa na nchi zote zilizopo Afrika Mashariki katika kutoa matibabu ya moyo hasa kwa watoto. 

Profesa Janabi amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya upimaji wa kugundua magonjwa ya moyo mapema kwa mtoto aliyeko tumboni mwa mama yake. 
"Tunafanya vizuri sasa katika ukanda wa Afrika mashariki, tunategemewa hasa katika oparesheni za magonjwa ya moyo kwa watoto," amesema.

Amesema hadi sasa wameshawatibu watoto kutoa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Komoro na Kenya.

"Tupo madaktari wa moyo 15, kati yetu watatu ni wa watoto, ili kuongeza idadi hiyo kuna weznetu wapo masomoni nchini Afrika Kusini na Israel hivi sasa," amesema.

Ameongeza "Changamoto kubwa tuliyonayo ni nafasi, tunahitaji jengo lingine, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameahidi kutupatia.

"Nia yetu tuwe na jengo maalumu kabisa kwa ajili ya watoto, hiyo itatupa fursa ya kufanya vitu vingi zaidi kuliko ilivyo sasa," amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement