Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Picha ya Catherine SunguraNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

SERIKALI imeweka utaratibu mpya wa kuwasajili katika fomu maalumu na kuwafuatilia hadi majumbani,  wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema jana kuwa utaratibu huo mpya umelenga kufuatilia mwenendo wa hali zao za afya kutokana na mlipuko wa  ebola nchini humoi, ulioripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) Mei 21, mwaka huu. 


Ummy alisema hadi sasa watu 43 wamegundulika kuugua na wanne wamefariki dunia. 

“Wananchi wasiwe na hofu, ebola haipo nchini, tunafuatilia kwa karibu na tumeimarisha mifumo ya ukaguzi. 
 Picha ya Alvin Daud
“Lakini wasafiri wanaotoka Kongo naomba wajue hatua hii haijalenga kuwabagua bali tunataka kulinda afya za Watanzania. 

“Watapimwa joto lao la mwili na watasajiliwa  katika fomu maalumu itakayotuwezesha kuwafuatilia kwa karibu, kwa sababu mtu anaweza kupimwa mara ya kwanza asionyeshe dalili, tunataka kuchukua tahadhari,” alisema. 

Waziri Ummy alisema   serikali imeagiza mashine nne za ukaguzi ambazo zitapelekwa   mipakani. 

Alisema   timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI zipo Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya na Songwe kushirikiana na wenzao  kwenye mikoa hiyo kupanga mikakati ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo. 

Binadamu huwa anapata virusi vya ebola kutoka kwa wanyama na   kuambukizana. 

Hata hivyo,  hadi leo watafiti hawajui kabla ya mnyama kupata virusi hivyo huwa vinaishi katika mazingira yapi.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement