moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Upatikanaji wa damu salama, dawa na uelewa mdogo wa jamii kuhusu ugonjwa wa selimundu mambo hayo matatu yametajwa kuwa ni changamoto zilizopo katika kukabili ugonjwa wa selimundu nchini.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangalla ameeleza hay oleo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Selimundu Duniani yaliyopewa kauli mbiu isemayo, Huduma bora za selimundu katika ngazi zote za kutolea huduma nchini’.

Dk. Kingwangalla akizindua kitabu hicho.

Dk. Kingwangalla ametumia fursa hiyo pia kuzindua rasmi kituo cha Shirikisho la la Vyama vinavyohudumia Wagonjwa wa Selimundu Tanzania (tanscda) na kitabu maalumu cha kuhifadhi taarifa za mgonjwa.

“Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha tunakabili ugonjwa huu, takwimu zinaonesha kila mwaka watoto kati ya 8,000 hadi 10,000 wanazaliwa wakiwa na ugonjwa huu,” amesema.

Dk. Kingwangalla akikata utepe kuzindua rasmi kituo hicho, (mwenye shati la kitenge) ni Joseph Mutaboyelwa ambaye amejitolea jengo hilo.

Amesema serikali imechukua hatua mbalimbali kukabili hali hiyo ikiwamo kuhamisha huduma za matibabu ya watoto hao kutoka kliniki za watoto hadi kliniki za magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ili wafuatiliwe kwa ukaribu.

Dk. Kingwangalla akisikiliza kwa makini ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wataalamu ndani ya kituo hicho.

Akizungumza, Kaimu Mkurugenzi tanscda, Elisha Osati amesema tafiti zinaonesha hadi sasa watanzania milioni sita wanaugua ugonjwa huo.
Picha ya pamoja.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement