NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Pedro Pallangyo amesema watoto wadogo nao huugua shinikizo la juu la damu.
Akizungumza na mtandao huu hivi karibuni, alisema mara nyingi hali hiyo hutokea iwapo wanakuwa wamepata magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani.
Daktari huyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na
Mafunzo wa JKCI alifafanua "Tatizo hili limegawanywa katika makundi mawili kuna ‘primary
hypertension’ na ‘secondary hypertension’.
"Tunaposema ‘secondary hypertension tunamaanisha
kwamba kunakuwa na kisababishi kingine ambacho kinapelekea mtu kupata shinikizo
la juu la damu," alisema.
Dk. Pedro alisema “Kwa mfano saratani au mvurugiko wa homoni kwenye damu na
mara nyingi hii ndiyo ambayo huwakumba watoto na kusababisha kupata shinikizo
la juu la damu.
Alisema “Lakini tunaposema ‘primary hypertension’ mara
nyingi huwakumba zaidi watu wazima, yaani hapa tunampima mgonjwa lakini
tunakuta hakuna tatizo lolote ambalo limesababisha wao kupata shinikizo la juu
la damu. Asilimia 95 ya pressure zote ni primary hypertension.
Alisema hata hivyo watoto ni nadra mno kupata tatizo hilo
na kwamba kwa mwaka huwa wanawapokea watoto watano wenye shinikizo la juu la
damu ikilinganishwa na watu wazima 400 hadi 500 ambao hufika katika taasisi
hiyo wakisumbuliwa na shinikizo la juu la damu.
Kumbuka: Kwa mujibu wa Katiba umri wa watoto ni kuanzia mwaka 0 hadi miaka 17
Kumbuka: Kwa mujibu wa Katiba umri wa watoto ni kuanzia mwaka 0 hadi miaka 17
Chapisha Maoni