Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

ALIYEKUWA Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Suleiman Kova ameipatia msaada wa vifaa vya kukabili majanga ya moto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) vyenye thamani ya Sh milioni 1.5.

Kamishna Kova amemkabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru hospitalini hapo leo.

Msaada huo unaojumuisha mitungi zaidi ya 10 na vifaa maalumu vya kutambua hali ya hatari iwapo moto unataka kutokea zaidi ya vitano, umetolewa na yake ya SUKOS ambayo inajishughulisha na utoaji Elimu kwa jamii jinsi ya kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwamo hayo ya moto.

Akizungumza Kamishna Kova amesema wameguswa kuipatia msaada Muhimbili kwani siku za hivi karibuni imekuwa ikitoa huduma bora ambazo wananchi wanaridhishwa nazo.


"Kabla ya kuja hapa tulifanya utafiti mdogo tumegundua, wananchi wanaridhishwa na huduma... kwa kweli Muhimbili is the best, naona tangu Rais John Magufuli alivyowapa maagizo wameyatii na kuyatekeleza, hongereni sana," amepongeza.

Amesema taasisi hiyo itaendelea kufanya kazi ya kuelimisha jamii na kutoa misaada ya aina hiyo kwa taasisi zingine pia ambazo zinatoa huduma bora kwa jamii.

Akizungumza Profesa Museru ameshukuru taasisi hiyo kwa msaada huo waliyoipatia Muhimbili na kwamba wametoa katika wakati mwafaka.
Mtaalamu akionesha jinsi kifaa cha kutambua iwapo janga la moto linataka kutokea, kinavyofanya kazi.


"Utatusaidia mno, sasa hivi tunafanya maboresho katika baadhi majengo yetu ambayo hayana vifaa vya kujikinga dhidi ya majanga ya moto," amesema.
Mtaalamu akielekeza jinsi ya kuzima moto kwa kutumia mtungi maalumu (fire extinguisher).

Kamishna Kova akifurahia jambo na Profesa Museru kabla ya makabidhiano hayo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement