Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
https://jamiihalisi.com/wp-content/uploads/2017/07/WEWWW-678x381.jpegNa Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam  

MKAZI wa Morogoro, Kitongoji cha Chaumbele, Rebeka Muya ambaye amejifungua pacha walioungana amesema kama inawezekana anatamani watoto hao watenganishwe.
 

Rebeka alisema hayo jana alipozungumza na mtandao huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wodi ya wazazi ambako amelazwa akipatiwa matibabu pamoja na watoto wake.
 

Alisema ujauzito wa watoto wake hao ni wa tisa na kwamba amebahatika kujifungua watoto wengine wanane ambao hawana kasoro yoyote.
 

“Nilipopewa taarifa na madaktari nimejifungua watoto hawa nilisikitika lakini mimi na familia yangu tumemuachia Mungu tukiamini atatusaidia,
lakini kama inawezekana natamani wataalamu wawatenganishe,” alisema.

 

Mama huyo alisema hata hivyo ikiwa jambo halitawezekana bado ataendelea kumshukuru Mungu kumjalia kupata watoto hao.
 

Akisimulia jinsi alivyolea ujauzito wa pacha hao, alisema ulimsumbua mno tofauti na ujauzito wa wanawe wanane wa kwanza.

“Nilianza kuhudhuria kliniki katika Zahanati ya Magubike iliyopo Morogoro Mei, mwaka huu mimba ikiwa na miezi sita pale walihangaika
kunipima lakini hawakuona watoto.

 

“Ikabidi wanipe rufaa kwenda Hospitali ya Misheni ya Berega ambapo walinifanyia uchunguzi kwa kutumia kipimo cha Ultra sound ikaonekana watoto walikuwa wamekaliana vibaya,” alisema.
 

Alisema ujauzito huo ulimsumbua kiasi kwamba alishindwa kula, kulala na wala kufanya jambo lolote.
 

Alisema ilipokabiria kipindi cha kujifungua alilazimika kuishi jirani na hospitali hiyo kipindi cha wiki tatu.
 

Aliongeza “Niliishi kwanza kwa majirani wiki mbili za kwanza, kisha nikalazwa wodini wiki moja iliyofuata ndipo nikajifungua, watoto wangu wakiwa wameungana,” alisema.
 

Msimamizi wa wodi hiyo, Suzana Ndambala alisema tayari madaktari wamechukua vipimo mbalimbali vya watoto hao sasa wanasubiri majibu.
 

“Ni mapema mno kueleza wamechukua vipimo gani, ambavyo wanavifanyia uchunguzi, pindi taarifa itakapokamilika wataeleza walichokibaini,”
alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement