Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image result for jkciNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

UZITO mkubwa na shinikizo la juu la damu ni matatizo ambayo yametajwa bado yanaonekana ni tishio na yanazidi kuwatesa wananchi walio wengi, huku wengi wakiwa hawajijui.

Kati ya watu 1,375 waliofika katika maonesho ya sabasaba na kupimwa afya zao asilimia 39.2 walikutwa na uzito mkubwa.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Pedro Pallangyo alisema hayo jana alipozungumza na
MTANZANIA.


 Alisema asilimia 31 kati ya watu hao 1,375 walikutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu.

“Wananchi hao walifika katika banda letu kule sabasaba, na walikuwa tayari kupima afya zao, wengi walikuwa hawajijui kama wana matatizo
hayo,” alisema.


Alisema kutokana na hali hiyo wagonjwa 39 walilazimika kuwapatia rufaa kufika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.

“Kati ya wagonjwa hao 39 ambao tuliwapa rufaa, wagonjwa 31 walikutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu na wagonjwa saba waligundulika
kuwa na moyo mkubwa na mmoja alikutwa na tatizo kwenye milango ya moyo wake (valve),” alisema.

Dk. Pallangyo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa taasisi hiyo alisema wagonjwa hao tayari wamepatiwa matibabu stahiki.

Alitaja dalili za mtu mwenye tatizo la shinikizo la damu kuwa ni kuhisi maumivu makali ya kifua hasa katika upande wa kushoto.

“Kwa kawaida mtu akifanya shughuli yoyote ile mwili huhitaji kiwango fulani cha damu, na mahitaji hayo hutofautiana kulingana na shughuli
anayoifanya lakini kwa mtu mwenye shinikizo la damu, hata akifanya shughuli ndogo huhisi uchovu wa mwili jambo ambalo si la kawaida,”
alisema.

Alisema zipo sababu nyingi zinazochangia mtu kupata tatizo la shinikizo la juu la damu, ikiwamo ulaji mbovu, kutokufanya mazoezi, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.

“Lakini kuna magonjwa kama vile kisukari, ambayo huweza kusababisha mtu kupata tatizo, lakini sababu nyingi zinaepukika hivyo naishauri
jamii kubadilika,” alishauri Daktari huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo watafiti vijana wa Kiafrika kwa mwaka 2017.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement