Shirika la Kimataifa la Save the Children limwakutanisha
jijini Dar es Salaam zaidi ya vijana 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
Bara na Visiwani,
Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano
wa Mwalimu Nyerere (JNICC), ambapo
vijana hao watajadili na kutoa mapendekezo yatakayoiwezesha serikali kuweka
mikakati yenye manufaa kuboresha afya ya vijana na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo wa siku tatu, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama amesema “Vijana ndiyo kundi kubwa kuliko makundi yote nchini, kwa
mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inaonesha wapo
milioni 16.2 kati ya watu milioni 44.
“Kwa mujibu wa Utafiti wa Nguvu Kazi uliofanywa mwaka 2014
ulionesha watu wenye uwezo wa kufanya kazi ni takriban milioni 25 na nguvu kazi
inayojishughulisha na shughuli za kiuchumi ni vijana kati ya umri wa miaka 15
hadi 35 sawa na asilimia 56,” amesema.
Amesema serikali ipo tayari kupokea mapendekezo
yatakayotolewa katika mkutano huo kwani yatasaidia kuboresha sera mbalimbali
zinazowalenga vijana.
“Tunawahitaji kwa Tanzania ya viwanda, hatuwezi kujenga
Tanzania ya viwanda ikiwa vijana wana afya duni, tunahitaji maoni yenu
yatusaidie kuboresha sera zinazowalenga vijana kwa mustakabali wa Taifa,”
amesema.
Makamu wa Rais wa Shirika la Global Health Save the
Children (USA), Robert Clay amesema “Tafiti zinaonesha vijana ni kundi kubwa
pia duniani, vijana ni Taifa la leo, mmepewa nafasi itumieni vema kutoa mawazo
yenu.
Chapisha Maoni