Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


https://c.ymcdn.com/sites/csme.site-ym.com/resource/resmgr/2016_Programs_/bigstock-Medicine-law-concep.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

ILI binadamu aweze kutimiza majukumu yake ya kila siku ni lazima awe na afya njema, inapotokea ameugua huhitaji kupata tiba dhidi ya ugonjwa unaomsumbua.

Kwa msingi huo, matibabu ni haki ya kila mtu ili aweze kuwa tena na afya njema lakini matibabu hayo anayopatiwa ni lazima yawe sahihi.

Miaka ya nyuma huduma za matibabu zilikuwa zikitolewa zaidi katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zinazomilikiwa na serikali.

Baadae tukashuhudia mashirika ya dini na taasisi mbalimbali nazo zikipata kibali cha kuanzisha huduma hizo za matibabu na hata watu binafsi.

Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania, Maulid Kikondo anasema hali hiyo imepelekea baadhi ya wamiliki kutoa matibabu kwa lengo la kufanya kibiashara zaidi kuliko kutoa huduma.

“Kwa kawaida mtu anapopatiwa matibabu huwa ni kwa nia njema, lakini kama ilivyo kwa mambo mengine ingawa ni jambo jema lakini kuna wakati matatizo mbalimbali huweza kujitokeza,” anasema.

Anasema matatizo hayo mara nyingi hujitokeza kati ya mtoa huduma na mpokea huduma.
 http://images.wisegeek.com/syringe-and-vaccine.jpg
“Hii ni kwa sababu wamiliki wengi (wa hospitali na vituo vya afya), wanatoa matibabu kwa lengo la kufanya biashara kuliko huduma, wanapokuwa na element ya biashara maana yake ni kwamba wanafikiria zaidi kupata faida.

“Unapokuwa na mfumo wa biashara kwenye matibabu huwezi kuwakwepa wajanja wajanja, kwa sababu siku zote, wafanyabiashara hutaka kutengeneza faida na hapa ndipo ‘yanapozaliwa’ matatizo.

“Kwa mfano unakuta mtu amekwenda hospitalini anajikuta anaandikiwa vipimo vingi ambavyo vingine wala havihitaji na kupewa dawa nyingi, kwa sababu mmiliki anahitaji kupata faida,” anabainisha.

Anasema ingawa si wamiliki wote wenye nia hiyo lakini kati ya wale walio waamini wanaofanya kazi kwa kuzingatia maadili wapo ambao hufanya kinyume.

“Miaka ya nyuma madaktari wengi walikuwa wakisoma hapa nchini na walikuwa rahisi hata kufahamiana na kujuana, tofauti na leo hii wengine wanasoma nje ya nchi na wanarudi kufanya kazi nyumbani,” anasema.

Anasema wakati walipokuwa wachache ilikuwa rahisi kujua na kukosoana pale ambapo mwenzao anakuwa amefanya makosa katika kutoa matibabu tofauti na sasa.

Anasema kutokana na hali hiyo ni muhimu sasa jamii kuanza kujifunza, kuifahamu na kuielewa vema sheria ya matibabu.

“Kutokana na matatizo ya ki-matibabu yanayoweza kujitokeza kati ya mtoa huduma na mpokea huduma, kilitengenezwa kipengele maalumu cha sheria kwa lengo la kuyatatua,” anasema.

Wakili huyo anafafanua “Wataalamu wa sheria walitengeneza ‘Medical legal’ ambayo baadae ilitumika kutengeneza kipengele cha ‘medical Negligence ambacho kazi yake ni kushughulika na haki za wagonjwa.
 https://www.bsoko.com/Adminpanel/productimage/1489578134$_32.jpg
“Yaani inapotokea mgonjwa amepata madhara yoyote wakati akipatiwa matibabu, kipengele hicho kinaeleza nani ambaye anawajibika kwa madhara hayo,” anabainisha.

Anaongeza “Kipengele hicho cha sheria kilitengenezwa makusudi, ili kulinda haki za mgonjwa, inaeleza wazi wakati gani daktari anapaswa kuwajibika pale ambapo inatokea anatoa matibabu kinyume na taratibu zilizowekwa.

Anasema hivyo sheria hiyo lengo lake kuu ni kusimamia na kulinda haki za mgonjwa kuhakikisha kwamba anapatiwa matibabu sahihi yanayostahili.

Jinsi inavyofanya kazi

Anasema jambo ambalo kila mtu anapaswa kulijua ni kwamba daktari anapaswa kupata idhini ya mgonjwa kabla ya kumpatia matibabu.

“Ili daktari awe na haki ya kutoa matibabu ni lazima pawe na idhini ya mgonjwa, mgonjwa aridhie mwenyewe na kabla ya kuridhia kutibiwa lazima pawe na majadiliano.

“Kwamba daktari anapaswa kumueleza kwa kina mgonjwa kwa mfano juu ya faida na madhara ya matibabu (dawa) au sindano atakayochomwa,” anasema.

Anaongeza “Lazima daktari amueleze mgonjwa ili aridhie mwenyewe iwapo apatiwe matibabu kwa dawa au sindano ambayo (daktari) amependekeza.

“Na mgonjwa anakuwa tayari anaelewa kwamba ingawa hiyo anayopatiwa ni tiba lakini labda inaweza kumsababisha athari nyingine kwenye mwili kwa mfano itapelekea figo zake kushindwa kufanya kazi baadae katika maisha yake na mambo mengineyo,” anasema.

Anaongeza “Lakini hapa kwenye idhini ya mgonjwa wakati mwingine huwa kuna utata, wapo watu ambao hudhani kwamba mgonjwa akisema sawa huku akiwa hajaelezwa faida na madhara ya matibabu anayopewa ni sahihi jambo ambalo si sawa.

“Sheria inataka lazima pawe na ‘informed concept’, mgonjwa lazima aelezwe na aelewe hasa huduma anayokwenda kupatiwa ni ipi ili atoe idhini yake,” anasema.
 http://www.dmu.ac.uk/webimages/study-images/courses/business-and-law/postgraduate/medical-law-and-ethics-llm-img-01.jpg
Anasema inapotokea kwa bahati mbaya kwamba mgonjwa ndiye ambaye amesaini fomu ya matibabu na hakukuwa na majadiliano ya kutosha kuelezwa juu ya kile anachokubaliana, iwapo atapata madhara moja kwa moja daktari aliyempatia huduma anaweza kushtakiwa kwa mujibu wa sheria hiyo.

“Madaktari wanaifahamu vema sheria hii na wengi wapo makini katika utendaji wao na ndiyo maana kabla ya kumuhudumia mgonjwa hufanya majadiliano kwa sababu akienda kinyume anaweza kushtakiwa kwa sheria hii,” anasema.

Anaongeza “Hata kabla daktari hajakuchoma sindano lazima akueleweshe kwa kina juu ya matibabu hayo na wewe mwenyewe uamue akutibu au la.

Anasema watu wengi wamekuwa wakipatiwa matibabu yasiyo sahihi na kuishia kupata madhara hata hivyo kwa kuwa hawana uelewa wowote kuhusu sheria hiyo wamekuwa wakiugulia majumbani mwao.

“Uelewa wa watanzania kuhusu sheria hii ni mdogo mno, wengi wanapata madhara na hawajui kwamba wanaweza kupata haki yao kwa kushtaki mahakamani, kesi zinazokuja mahakamani ni chache mno, mataifa yaliyoendelea wanaitumia sheria hii kudai haki zao,” anabainisha.

Lazima uandaliwe kisaikolojia

Wakili maulid Kikondo anasema ingawa sheria inatambua kwamba mgonjwa anapochukua uamuzi wa kukaa mbele ya daktari ni hatua ya kuridhia pia lakini kuna matibabu ambayo daktari anapaswa kumuandaa kisaikolojia mgonjwa kabla ya kumtibu.

“Kwa mfano mgonjwa ni wa jinsi ya kike na daktari ni mwanamume ikiwa itabidi avue nguo kwa mfano ili atibiwe ni lazima daktari amueleze mapema ili ajiandae kisaikolojia,” anasema.

Anasema kwa kuwa mgonjwa ana haki na maisha yake ataamua mwenye iwapo apatiwe matibabu hayo au la na kwamba daktari hapaswi kumlazimisha.
 http://www.medhatsoliman.com/wp-content/uploads/2015/10/Medical-law-in-UAE-The-Medical-Compensation.jpg
Matibabu kwa mtoto

Anasema ni makosa daktari kumtibu mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 kabla ya kupata idhini kutoka kwa wazazi au walezi wake.

“Ndiyo maana kabla ya kumfanyia matibabu yoyote mtoto chini ya miaka 18 lazima wazazi wake waitwe, wao watatoa idhini kwa niaba yake,” anafafanua.

Mgonjwa aliyezidiwa

Wakili huyo anasema taaluma inampatia haki daktari kumsaidia na kumuhudumia mgonjwa aliye katika hali mbaya ambayo inaweza kupelekea kupoteza maisha bila kusubiri idhini yake.

“Yaani kwa mfano, mtu amepata ajali na kufikishwa haraka hospitalini, daktari ana haki ya kumsaidia bila kusubiri majadiliano na idhini ya mgonjwa, lakini anachopaswa kufanya (daktari) ni kutibu tatizo lilompelekea mgonjwa kufikishwa hospitalini.

“Kwamba labda anajeraha linatoka damu nyingi, atatibu jeraha hilo pekee ikiwa mgonjwa huyo ana tatizo jingine kwa mfano aliwahi kuumia jicho lake huko miaka ya nyuma, daktari hana haki kumtibu kwa wakati huo kwa sababu mgonjwa hajaridhia,” anasema.

Sheria msumeno

Anasema wakati sheria hiyo ikilinda haki za mgonjwa wakati mwingine pia hulinda haki za daktari anayempatia matibabu.

“Kwa mfano, daktari amepokea majeruhi wa ajali amempatia huduma lakini kwa bahati mbaya majeruhi huyo akafariki dunia na ndugu wakalalamika kwamba daktari amesababisha kifo cha ndugu yao.

“Tutasikiliza maelezo ya pande zote mbili, ikiwa mgonjwa huyo alifariki wakati daktari akitimiza wajibu wake wa kumsaidia kuokoa maisha kwa kutibu tatizo lililokuwa likihatarisha uhai wake, basi daktari husika anakuwa huru.

“Lakini ikiwa mgonjwa alifariki wakati daktari akitibu tatizo jingine ambalo halihusiani na ajali hiyo, bila idhini ya mgonjwa hapo daktari anakuwa matatani na atahukumiwa kwa mujibu wa sheria,” anafafanua.

Makala haya kwa mara ya kwanza yamechapishwa Agosti 31, mwaka huu kwenye gazeti la MTANZANIA

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement