Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
http://m.ippmedia.com/sites/default/files/articles/2017/05/18/malaria.jpgPicha na mtandao

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
 
JAMII imeshauriwa kuondokana na dhana potofu iliyojengeka kwamba kulala ndani ya chandarua ni hatari na kunasababisha upungufu wa nguvu
za kiume.

Rai hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Mbu waenezao malaria wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Charles Mwalimu alipozungumza kwenye semina ya siku moja ya kuwapa uelewa waandishi wa habari kuhusu hali ya malaria kwa sasa nchini.

“Katika baadhi ya mikoa tumepata changamoto tulipokwenda kusambaza vyandarua, watu wanaamini kwamba chandarua kinasababisha upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo si kweli,” alisema.

https://www.yumpu.com/xx/image/facebook/48124555.jpg 
Alisema hadi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika duniani kuthibitisha juu ya jambo hilo.
“Hakuna uthibitisho, lengo la serikali ni kuwalinda raia wao na si kuwaangamiza, na vyandarua vinavyogawiwa kwa wananchi vimethibitishwa
na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Taasisi ya Usajili wa Viuatilifu katika Kanda za Joto (TPRI) kuwa ni salama,” alisema.

Alisema pamoja na changamoto hiyo, nyingine ni kwamba wapo wengine ambao wanaamini kwamba kulala ndani ya chandarua ni sawa na kulala
ndani ya jeneza.

“Wengine wanadhani kwamba ni imani za freemason, hivyo hawaoni sababu ya kuvitumia, ni vema wakabadili mtazamo kwani kutumia chandarua kuna faida nyingi hasa kupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa malaria,” alisema.

Aliongeza “Pamoja na faida hiyo ya kupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa malaria jambo jingine ni kwamba mtu hupata usingizi mnono.

Alisema Wizara imejipanga kufanya kampeni ya kusambaza vyandarua kuanzia mwakani kwenye mikoa yote 26 ili kuendeleza mapambano dhidi ya
ugonjwa huo.

“Fedha zipo tutapata kutoka, Mfuko wa Dunia wa kukabiliana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu, katika mikoa 11 tutagawa vyandarua takriban
milioni 15 lengo chandarua kimoka kwa kila watu wawili,” alisema.

Awali akizungumza, Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi na Matibabu, Mpango wa  Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dk. Siasbert Mkude alisema tafiti zinaonesha kiwango cha maambukizi cha ugonjwa huo ni kikubwa katika maeneo ya vijijini.

“Tafiti zinaonesha pia maambukizi ya malaria yapo kwa kiwango cha juu katika familia zenye maisha duni, unaonekana ni ugonjwa wa watu maskini, upuliziaji wa dawa ukoko na matumizi ya vyandarua yatasaidia kukabili hali hii,” alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement