Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry Charles akisisitiza jambo
huku akionyesha kitabu hicho ambacho kitakuwa kikitumika wakati wa
kuwahudumia watoto hao.
NA VERONICA ROMWALD - DAR ES SALAAM
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili (MNH) imezindua mwongozo maalum utakaotumika kuhudumia
watoto wachanga wanaozaliwa na matatizo mbalimbali hata katika hospitali
nyinginezo nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Daktari Bingwa wa
Watoto Wachanga wa Muhimbili, Edna Majaliwa alisema mwongozo huo umetengenezwa
ili kuendana na hali ya sasa kwani ule ulipo umepitwa na wakati.
Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye mkutano wa kuzindua kitabu
kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga baada ya kuzaliwa.
“Tulikuwa
na mwongozo lakini ulitengenezwa miaka mingi iliyopita, tukaona tunahitaji
mwongozo mpya ambao ndiyo huu tunaozindua leo (jana), Kwa kuwa Muhimbili ni
hospitali ya rufaa na tunapokea wagonjwa wengi kutoka katika hospitali
mbalimbali.
“Hivyo,
tuliona tunahitaji kama Taifa kuwa na mwongozo wa pamoja ambao utasaidia kutuongoza
katika kuhudumia watoto wachanga wanaozaliwa na matatizo mbalimbali,” alisema.
Alisema
takwimu zinaonesha watoto wachanga wamekuwa wakizaliwa na matatizo mbalimbali
huku wengine wakiwa hawajatimiza umri wa miezi tisa kama inavyopaswa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho
“Kuna
visababishi vingi vinavyochangia hali hiyo kwa mfano chanzo kikuu tunaona ni
maambukizi katika njia ya mkojo (hasa U.T.I), kifafa cha mimba, uzazi wa pacha,
shinikizo la damu, kisukari na magonjwa mengineyo,” alisema.
Aliongeza
“Hivyo ni vizuri mama kuwahi kliniki pindi tu anapojihisi kuwa ni mjamzito ili
afanyiwe uchunguzi na kupewa ushauri unaostahili ili aweze kujifungua mtoto
mwenye afya njema.
Naye,
Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alisema “Hospitali kubwa kama
Muhimbili ni vizuri ikiwa na miongozo ya namna hii hata nchi za ulaya wenzetu
wana miongozo inayowasaidia kuwaongoza katika kutoa matibabu mbalimbali.
MWISHO
Chapisha Maoni