Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
http://topyaps.com/wp-content/uploads/2015/09/Synthetic-pads.jpgNA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

KITENDO cha mwanamke kutumia taulo ya kike kwa muda mrefu kujihifadhi wakati wa kipindi cha hedhi pasipo kubadilisha, kunaweza kumsababishia kupata magonjwa mbalimbali yakiwamo ya moyo.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Bashir Nyangasa amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya moyo duniani, yanayofanyika  Septemba 29, kila mwaka (leo).

“Kipindi cha hedhi ni muhimu mwanamke awe msafi ahakikishe anabadilisha ile pedi anayotumia kujihifadhi na si kukaa nayo kwa muda mrefu, ni hatari.

“Unapokaa na pedi kwa muda mrefu, ile damu ikajaa pale hutengeneza bakteria (wadudu), hapo unahatari ya kupata maambukizi kwenye kizazi, wale wadudu wanaweza kusafiri kwenda kuathiri moyo au figo zako,” amesema.
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2017/01/Bashiri-Nyangassa-225x300.jpg
Dk. Nyangasa (anayezungumza pichani) ameongeza “Hiyo tunaita ‘entry point’ yaani hata ukijikata wadudu wanaweza kusafiri kwenda kwenye moyo wako na kuuathiri, hivyo ni muhimu kuzingatia usafi katika kipindi hicho.

Naye, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Tulizo Shemu ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi, kufika katika Taasisi hiyo hii leo.

“Tutafanya upimaji bure na tutatoa elimu ya lishe, jinsi ya kujikinga na magonjwa ya moyo, kuanzia saa mbili hadi saa 10 jioni bila gharama yoyote,” amesisitiza.
http://www.jkci.or.tz/uploads/gallery/large_1473174606-jengo%20croped.jpg
Ameongeza “Kuanzia Septemba 25 hadi 29, mwaka huu tayari tumewafanyia upasuaji wagonjwa 23 kwa kushirikiana na madaktari wenzetu kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika, JKCI tunafanya maadhimisho haya kwa kushirikiana pia na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF).

“Wananchi watapimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na  kupewa ushauri. Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu. Kauli mbiu ya siku hii ni:  “Moyo wenye Afya”,” amebainisha.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement