*Ni sehemu ya maadhimisho Siku ya Moyo Duniani yanayofanyika kila mwaka Septemba 29, mwaka huu (kesho)
NA MWANDISHI MAALUMU - DAR ES SALAAM
WITO
umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani kujitokeza kwa
wingi, kufika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo leo watatoa
elimu ya lishe, jinsi ya kujikinga na magonjwa ya moyo.
Rai
hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo,
Tulizo Shemu alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya
Moyo Duniani yanayofanyika kila ifikapo Septemba 29, kila mwaka (kesho).
“JKCI
tumekusudia kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa kila mtu ambaye atafika
kesho (leo) kuanzia saa mbili hadi saa 10 jioni bila gharama yoyote, kuanzia Septemba
25 hadi 29, mwaka huu tayari tumewafanyia upasuaji wagonjwa 23 kwa kushirikiana
na madaktari wenzetu kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika,” amesema.
Amesema
JKCI wanafanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana pia na Chama cha Madaktari wa
Moyo Tanzania (THF).
“Wananchi
watapimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Kwa wale watakaokutwa na matatizo
ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu. Kauli mbiu ya siku
hii ni: “Moyo wenye Afya”,” amebainisha.
Chapisha Maoni