Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
WAKILI
wa Mahamaka Kuu Tanzania, Maulid Kikondo amesema kifo chochote kinapotokea kwa
kutatanisha ni lazima uchunguzi ufanyike kabla ya mwili wa marehemu kuzikwa.
Amesisitiza
ni makosa ndugu kufanya maziko bila kupata taarifa ya daktari inayoeleza sababu
iliyopelekea kifo hicho kutokea.
Wakili
Kikondo amesema hayo alipozungumza na matukionamaisha katika mahojiano maalumu
ikiwa ni muendelezo wa mazungumzo kuhusu Sheria ya Matibabu.
“Kosa
kubwa ambalo naona watu wengi wamekuwa wakilifanya ni kuogopa au kukwepa
kuhudhuria kipindi mwili wa marehemu unapokuwa unafanyiwa uchunguzi,” amesema.
Amesema
kitendo hicho kinasababisha kushindwa kujua nini hasa kimepelekea kifo chake
iwapo ni uzembe uliotokana na wataalamu wa afya au la.
“Matibabu
yanapaswa kuwa professional, kwa mfano unapomfikisha mgonjwa wako hospitalini
akapoteza maisha ndani ya saa 24 akipatiwa matibabu ni lazima mjue nini
kinasababisha kifo chake.
“Lakini
bahati mbaya, watu wengi huogopa kuhudhuria kwenye 'postmotum' matokeo yake ni
kwamba hamtajua ukweli kuhusu kifo hicho,” amebainisha.
Ameongeza
“Ikiwa kimesababishwa na uzembe wa daktari, kwa kuwa mmeogopa anaweza kutumia
mwanya huo kutengeneza taarifa isiyo ya kweli na ninyi makosa hali ya ndugu
yenu.
Chapisha Maoni