TAASISI
ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) inakabiliwa na
uhaba wa vyumba vya upasuaji ili kutosheleza mahitaji yake.
Akizungumza
jana hospitalini happy wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kujitolea
Duniani ambapo pia alipokea msaada was fedha na vifaa mbalimbali
kutoka Taasisi ya Foundation for Civil Society, MkurugenziBoniface
alisema hivi sasa wanavyo vyumba sita pekee.
"Kwa
taasisi hi tunahitaji kuwa navyo angalau 15 ili kutosheleza na pia
tunatamani tungekuwa na chumba kimoja kwa ajili ya watoto pekee,
asilimia 60 ya wagonjwa wetu huhitaji upasuaji," alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo wanalazimika kufanya upasuaji kwa watoto wenye
tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi hasa jumamosi.
"Huwa tunawafanyia Kati ya watoto 20 hadi 50 kwa siku na wakati mwingine tunalazimika kufanya hadi usiku," alisema.
Aliishukuru
serikali kwa kuendelea kuijengea uwezo taasisi hiyo pamoja na wadau
mbalimbali wanaoendelea kusaidia ukiwamo Ubalozi was Kuwait nchini.
"Serikali
ina nia ya dhati kuboresha sekta ya afya, wadau wakiwamo Jumuiya Khoja
Shia Ithna Asher nao wamekuwa wakifadhili matibabu ya watoto ambapo hadi
sasa tumefanya kambi 20 na watoto 400 wamenufaika.
"Shughuli
hizi ili tufanikishe tunahitaji damu ya kutosha, ubalozi wa Kuwait
ulitupatia benki ya damu, hivyo natoa rai kwa wananchi kuja pia
kujitolea damu ili kwa pamoja tufanikishe matibabu haya," alisema.
Dk.
Boniface aliishukuru Taasisi ya Foundation for Civil Society kwa
kuungana na taasisi hiyo katika kuwezesha matibabu ya watoto wenye
vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Awali,
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Francis Kiwanga alisema wapo
tayari kuwakatia bima ya afya watoto 50 wenye matatizo hayo wanaotibiwa
hospitalini hapo.
"Leo
(jana) tunakabidhi pia msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya zaidi
ya Sh milioni 15 ikiwamo mchele, mafuta ya kupikia, sabuni za kuogea,
nepi za kisasa (parmpas), mafuta ya kupaka, magodoro na vinginevyo.
"Pamoja
na hivyo, tunakabidhihundi yenye thamani ya Sh milioni nane
zitakazowezesha matibabu ya upasuaji kwa watoto 100 wenye tatizo hilo,"
alisema.
Chapisha Maoni