Na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubsya akimsikiliza daktari wakati wa ziara yake hiyo.
Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Taasisi ya
Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)
imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha
wagonjwa nje nchi kufuataia kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali
zilikua hazipatikani hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt Mpoki
Ulisubisya alipofanya ziara katika taasisi hiyo ili kujiridhisha shughuli za utoaji huduma katika taasisi hiyo.
Akizungumza na menejimenti ya MOI Dkt Ulisubisya amepongeza kazi nzuri
na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za
kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.
"Mnafanya kazi
nzuri sana , jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu,
naomba muongeze ubunifu zaidi. Hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda
huu wa Afrika pekee bali duniani. Hii ni changamoto kwetu sote
kuifikisha hapo," amesema Dkt Ulisubisya.
Chapisha Maoni