Mkurugenzi wa MOI, Dk. Respicious Boniface
(katikati) akipokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Spectrum
Hamza Algabri.
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
TAASISI ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu,
Ubongo, Mgongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI) imepokea msaada wa dawa za
binadamu zenye thamani ya Sh milioni 16.84.
Dk. Boniface akizungumza katika kikao hicho.
Msaada wa dawa hizo umetolewa na kampuni ya usambazaji dawa Wide Spectrum ya nchini Misri.
Kikao cha makabidhiano kikiendelea
Akipokea msaada huo, Mkurugenzi wa MOI, Dk.
Respicious Boniface aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia dawa hizo kwani
zitawasaidia kutoa huduma kwa wale wenye uhitaji.
Naye,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wide Spectrum, Hamza Algabri aliipongeza MOI kwa
huduma za upasuaji ambazo wamekuwa wakiwafanyia wananchi wanaohitaji na kwamba
wapo tayari kuendelea kushirikiana nao zaidi.
Tunashukuru sana
Picha zote na Veronica Romwald
Chapisha Maoni