Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri  (pace maker) ikiwa ni sehemu ya  mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na  kampuni ya Medtronic  tawi la  Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.


Profesa Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi  mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG)  unavyofanya kazi mwilini wakati wa mafunzo hayo yanayoenda sambamba na vitendo  ya siku tano   yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto (mwenye kipaza sauti), Sulende Kubhoja akiuliza jambo wakati wa mafunzo hayo.

Wafanyakazi wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Ahmed Osman (hayupo pichani)  kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha jinsi  mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG)  unavyofanya kazi mwilini.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement