Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Dk. Respicious Boniface (aliyesimama pichani) ameihakikishia Bodi ya wadhamini ya taasisi hiyo
kwamba wataendelea kufanya kazi kwa weledi mwaka 2018.
Amesisitiza
watafanya hivyo ili kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora kwa
wakati muafaka.
Dk.
Boniface alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao kati ya wafanyakazi,
viongozi waandamizi wa MOI na wajumbe wa bodi hiyo.
Awali
akizungumza wakati akitoa salamu za kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka
2018, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Zakia Meghji (Pichani) aliwapongeza wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwahudumia
watanzania waliopata matatizo mbalimbali hasa kutokana na magonjwa ya ajali.
Alisema
anatambua kazi kubwa na ngumu wanayofanya madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa
vitengo mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania wanaofikishwa katika taasisi
hiyo.
“Natambua
kazi kubwa inayofanyika hapa usiku na mchana ili kukabiliana na ongezeko la
wagonjwa wanaotokana na ongezeko la ajali hapa nchini,” alisema.
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.
Aliongeza
“Sisi kama Bodi tunatambua kazi kubwa na nzito mnayofanya, kwa waliopo nje ya
MOI si rahisi kutambua hilo. Nawapongezeni sana, na niwatie moyo kwamba
tutashirikiana ili kupambana na changamoto zinazojitokeza.
Alisema
ana imani kwamba kazi kubwa zilizofanyika mwaka 2017 zitaendelea na kuboreshwa
zaidi katika mwaka 2018 ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora hapa
hapa nchini.
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.
Aliishukuru
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kurahisisha
upatikanaji wa vifaa, vifaa tiba na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya
wagonjwa na watoa huduma.
Wafanyakazi wa MOI, wakisikiliza jambo kwa makini wakati wa kikao hicho.
Naye,
Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Bakari Lembariti aliwapongeza
wafanyakazi hao kwa kuendelea kutimiza dira ya MOI kuwa Kituo cha Weledi Afrika
na kuendeleza ubunifu katika utoaji huduma ambazo hazifanyiki katika nchi
nyingi za kiafrika.
“Hatua
hiyo imeifanya MOI kuwa Kituo cha Weledi Afrika katika tiba ya Mifupa, upasuaji
wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, mnastahili pongezi,” alisema.
Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyakazi hao akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha Uhusiano na Ustawi wa Jamii MOI
Chapisha Maoni