Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli
Na Mwandishi Maalum, Switzerland
Tanzania imetajwa kuwa nchi bora katika Bara la Afrika
kwa kuwa na Uchumi Jumuishi (Inclusive Economy) katika Mkutano wa Uchumi
Duniani (World Economic Forum).
Tanzania inaongoza nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi ya Ghana na Cameron.
Mkutano huo ulifanyika Davos Switzerland kuanzia Januari 23 hadi 26, mwaka huu.
Kupitia
taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari mapema leo, Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Kuinua Diplomasia ya Uchumi Tanzania (TEDEF), Dk.
Telesphory Kyaruzi (Pichani) amesema hatua hiyo ni kubwa na ya kupongeza.
"TEDEF
tunaungana na World Economic Forum kumpongeza Rais John Magufuli kwa
hatua hii, ambayo imechangiwa na serikali anayoiongoza kuhimiza watu
kufanya kazi halali ili kujipatia kipato.
"Aidha,
kuhimiza kila mwananchi anayeshiriki kufanya shughuli za kiuchumi
kuhakikisha analipa kodi na hivyo kupata fursa sawa za kiuchumi,"
amesema.
Dr Kyaruzi
ameongeza "Tanzania itaendelea kukua kiuchumi kutokana na maono
aliyonayo Rais Magufuli hususan kufikia Tanzania ya uchumi wa kati kwa
kutumia rasilimali tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Chapisha Maoni