Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri Ummy akikagua ramani ya kituo cha afya kilichojengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Subi na kushoto ni mmoja wa viongozi wa Shirika hilo.

Na.WAMJW,Mwanza

Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia Fedha za kuboresha huduma za dharura zinazotolewa na Serikali zitumike ipasavyo na si kwa matumizi mengine

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  jijini hapa wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya pamoja na ujenzi wa huduma za dharura za Uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Igombe Wilayani Ilemela
Waziri Ummy alimpongeza Mkurugenzi wa Ilemela kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambapo alijionea kazi nzuri inayoendelea katika kituo hicho ambapo wametumia wajenzi wa kawaida na ujenzi huo unaenda vizuri na kwa kiwango kinachoridhisha

Aidha,alisema Fedha za kuboresha miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura zitumike kama haya angalau kujengwe chumba cha upasuaji,maabara ya damu na tunamataka wodi ya wazazi na nyumba moja ya mtumishi kuliko kujenga masuala mengine
“kama fedha zitabaki unaweza kufikiri kujenga vitu vingine,kuliko kqenda kutumika kwa masuala mengine kama baadhi ya sehemu nyingine wanavyofanya, kama fedha zimebaki nipo tayari kukuruhusu kujenga kitu kingine Mkurugenzi,hongera sana Mkurugenzi na viongozi wengine”.

Hata hivyo alisema Tanzania ni moja ya nchi yenye vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto”leo hii toka saa sita usiku tuanze siku hadi saa sita usiku wanawake 30 wa kitanzania wanafariki kwa sababu tu ya kutimiza wajibu wao wa kuleta kiumbe duniani”
“Kwahiyo Mhe.Rais alichokifanya  kwa kushirikiana na wadau tunaboresha huduma za uzazi zikiwepo za upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,hivyo tumefurahi kuona hapa zile zshilingi milioni mia tano zimetumika ipasavyo,binafsi nimedhirika  na kazi iliyofanywa hapa karume hivyo naahidi kuleta fedha kwa ajili ya   kuboresha miundombinu ya kituo cha afya Buzurugwa”alime Waziri Ummy

Wakati huo huo nae naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemele Dkt.Angela Mabula alisema wao kama viongozi watahakikisha fedha zote zitakazoenda kwa ajili ya afya itatumika ipasavyo na wataisimamia ili kuweza kuboresha miundombinu ya sekta ya afya

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amewataka wananchi wa    Igombe kuendeleza mshikamano wanaouonyesha ili kuendelea kufanya makubwa zaaidi kwa kujiletea maendeleo”mchakato wa maendeleo chini ya Jemedari wetu rais Magufunli ndo kwanza umeanza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement