NA VERONICA ROMWALD - DAR ES SALAAM
UGONJWA wa ukoma bado umeendelea kuwa tatizo la kiafya nchini ambapo idadi ya kiwango cha ugunduzi wa wagonjwa kimeongezeka.
Mwaka
2006 kiwango cha ugunduzi kilikuwa mgonjwa mmoja kati ya wagonjwa
100,000 ambacho kimeongezeka kufikia wagonjwa wanne katika watu 100,000
mwaka 2016.
Hayo
yalielezwa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile
alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukoma
Duniani yanayofanyika Januari 28, kila mwaka.
"Takwimu
za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma za mwaka 2016
jumla ya wagonjwa wapya 2,047 waligundulika, takwimu hizo zinaifanya
Tanzania kuendelea kuwa miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa
ukoma duniani," alisema.
Alisema takribani mikoa yote nchini inagundua na kutibu wagonjwa wa ukoma japo kwa viwango tofauti.
"Hivi
sasa bado kuna mikoa kumi ambayo inagundua wagonjwa wapya kila mwaka,
mikoa hiyo ni pamoja na Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani, Tanga, Geita,
Dodoma, Tabora na Kigoma," alitaja.
Alisema
bado pia zipo Wilaya 20 ambazo kiwango cha ukubwa wa tatizo la ukoma
kipo juu mno na kwamba bado hazijafikia lengo la utokomezaji.
"Wilaya
hizo ni Liwale, Nkasi, Ruangwa, Nanyumbu, Shinyanga, Kilombero, Mafia,
Pangani, Mvomero, Masasi mjini, Lindi vijijini, Kilwa, Mpanda,
Nachingwea, Rufiji, Korogwe, Mkinga, Ulanga, Morogoro vijijini na
Chato," alitaja.
Dk.
Ndungulile alisema takwimu za miaka 10 iliyopita kuanzia 2007 hadi 2016
zinaonesha watoto wapatao 1,456 waligundulika na kutibiwa ukoma.
"Miongoni
mwa watoto hao 73 waligundulika wakiwa tayari wamepata ulemavu wa
kudumu, yaani wakiwa tayari wamekatika baadhi ya viungo vyao na wengine
kuhitaji kutumia viungo bandia," alisema.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'Tokomeza Ukoma Kuzuia Ulemavu Miongoni mwa Vijana Wetu.
Chapisha Maoni