Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image result for WANANDOANA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
FURAHA ya binadamu aliyekamilika hapa duniani ni kupata mtoto hasa wale ambao wamekubaliana kuishi pamoja (wanandoa) hata hivyo miaka ya hivi karibuni wengi wanakabiliana na matatizo ya uzazi.
Tunashuhudia baadhi ya ndoa ‘zikivunjika’ na ‘kusambaratika’ kutokana na wanandoa husika kukosa (kushindwa) kupata watoto, ni jambo linalohuzunisha.
Mara nyingi wanawake ndio ambao hutupiwa lawama kwenye jamii inapotokea changamoto hiyo hata hivyo wataalamu wa afya wanaeleza kwamba hata wanawaume wanaweza kuchangia hali hiyo.
Zipo pia simulizi za ndugu, jamaa na marafiki ambao hulazimika kwenda nje ya nchi kufuata matibabu ya kibingwa ili kupandikiza ujauzito.
Matibabu hayo ni gharama kubwa si wananchi wote wanaokabiliwa na tatizo hilo huweza kuzimudu isipokuwa wale tu wenye uwezo mkubwa kifedha ndiyo ambao hufanikiwa kugharamia.
Hatua ya Hospitali ya Kairuki kukusudia kuanzisha huduma hiyo nchini imepokewa kwa furaha nchini huku wengi wakisema itasaidia kuokoa ndoa nyingi.
“Binafsi nilivyosikia kuhusu huduma hiyo, nimefarijika mno, nina marafiki zangu ambao wamepitia changamoto hiyo kwa hivyo ikianza nchini wengi watapata watoto,” anasema Mussa Jumanne Mkazi wa Mbezi Luis jijini hapa.
Uongozi wa Hospitali ya Kairuki (KH), Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN), Hospitali ya Kairuki (KH)  na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki  (KHMU) unakusudia kuanzisha huduma hiyo nchini ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya Hubert Kairuki aliyefariki mwaka 1999.What AI Can Do for IVF
Mwasisi huyo alifariki dunia wakati miradi yake hiyo ikiwa michanga na sasa imekuwa kimbilio la wananchi wengi. 
Daktari Clementina Kairuki anasema kwa kawaida iwapo mke na mume wanahitaji kupata mtoto wanapaswa kushiriki tendo la ndoa mara mbili hadi tatu kwa wiki.
“Wanapaswa kushiriki vema tendo la ndoa na ikiwa watashiriki kwa kipindi cha mwaka mmoja huku wakiwa hawatumii kinga yoyote lakini wakashindwa kupata mtoto hapo tunaanza kufanya uchunguzi wa awali kwanini hali hiyo ipo.
“Hapo tunaanza kuhesabu kwamba kuna tatizo limeanza na tunaanza kufanya uchunguzi, kwa sababu katika kipindi cha mwaka mmoja wanakuwa na uwezekano wa kupata mimba kwa kiwango cha asilimia 86.
“Hivyo kipindi cha mwaka wa kwanza huwa ni cha kusubiri lakini ikiwa watakaa zaidi hadi mwaka wa pili hapo inabidi tuwafanyie uchunguzi wa kina zaidi na huwa tunaangalia vitu vingi mno ikiwamo ushiriki wao katika tendo,” anasema.
Ukubwa wa tatizo
Anasema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuna watu milioni 48 duniani ambao wanakabiliwa na tatizo la kutopata ujauzito.
“Lakini matokeo hayo yalikuwa ni ya uchunguzi wa watu ambao walikaa kwa kipindi cha miaka mitano bila kupata ujauzito, huku tafsiri ni kwamba inabidi wawe wamekaa miaka miwili bila kupata ujauzito hivyo WHO mwaka 2014 likasema kwamba kwa waliokaa miaka miwili hadi miwili na nusu maana yake watu milioni 12 ndiyo wenye tatizo la kutopata ujauzito,” anasema.
Anasema kutokana na matokeo ya utafiti huo WHO ilitangaza tatizo hilo kuwa ni janga.Fertilised Ivf Embryo Acrylic Print
“Hapa nyumbani (Tanzania) upo tuna matokeo ya utafiti ambao ulifanyika zamani kidogo ambao unaonesha asilimia 20 ya mtu mke na mume walio katika umri wa kupata ujauzito wanakabiliwa na changamoto hiyo,” anasema.
Anasema katika kliniki yao Kairuki asilimia 30 ya wanawake na wanaume wanaowahudumia wanakabiliwa na tatizo hilo.
“Katika hao, asilimia mbili hadi 10 wanashindwa kabisa kutatuliwa matatizo yao na hivyo kujitaji njia mbadala (ya upandikizaji) ili waweze kupata watoto,” anasema.
Anasema changamoto wanayoiona ni kwamba mara nyingi wanawake ndiyo ambao hujitokeza na kugundulika mapema huku wanaume wakija baadae kuhudhuria kliniki.
Visababishi
“Wote wanapaswa kuchunguzwa, mwanaume anaweza kuchangia tatizo hili kwa asilimia 40 hadi 50 na wanawake huvyo hivyo huku kwa asilimia tano tu wanaweza kuchangia wote wawili kushindwa kusababisha ujauzito,” anasema.
Dk. Kairuki anasema tafiti zinaonesha wanawake wengi nchini hushindwa kupata ujauzito kutokana na kuziba kwa mirija ya uzazi kuliko wakina baba.
“Kuziba kwa mirija ya uzazi kunaweza kusababishwa na sababu nyingi, ikiwamo kutoa mimba ovyo, kujifungua katika mazingira ambayo si salama kunaweza kusababisha maambukizi na hatimaye kuziba mirija ya uzazi.
“Watu wanatoa ovyo mimba kama hatasafishwa vizuri hupata ‘infection’ ambazo baadae husababisha mirija ya uzazi kuziba, au mama anachelewa kujifungua anapelekwa chumba cha upasuaji na kufanyiwa upasuaji haraka haraka kutoa mtoto pia anaweza kupata ‘infection’,” anabainisha.
Anasema wapo wengine ambao wamezaliwa na matatizo ya homoni kwamba zinakuwa hazija-‘balance’ inavyotakiwa na hivyo kushindwa kupata ujauzito au kusabisha ujauzito.
“Mtu anaweza pia kuwa amezaliwa huku viungo vyake vya uzazi vikiwa havijakamilika na kujikuta akishindwa kusababisha au kubeba ujauzito lakini pia mtu anaweza akashindwa kupata ujauzito kutokana na maradhi mbalimbali ikiwamo saratani au fibroids (uvimbe kwenye kizazi.
“Hata hivyo kuna asilimia 15 ya wana-ndoa ambao hawapati ujauzito na sababu hazijulikani yaani ukiwachunguza unakuta hawana tatizo lolote na wanashiriki vema kabisa tendo,” anasema.
Ubora wa mbegu
Dk. Kairuki anasema kwa upande wa wanaume huwa wanaangalia vitu vinne ikiwamo ubora wa mbegu zake.
“Ule wingi wa mbegu anatakiwa kutoa mara moja kiwango chini ni milioni 39 kwa mkupuo wa kwanza, ile kasi yake inapaswa kuwa angalau asilimia 32 na ‘concentration’ katika ujazo huo iwe mililita moja inapaswa kuwa chini ya milioni 15,” anabainisha.
Anasema huwa wanaangalia pia umbo la mbegu zake jinsi zilivyokaa.
“Tukichunguza tunajua iwapo zipo sawa sawa zinavyopaswa au la, unaweza kukuta baba hana mbegu kabisa au zipo chache na hazikidhi kiwango kinachotakiwa.
“Hii inatokana na mambo mengi hasa kama zile ‘chromosome’ zake hazipo sawa sawa au anakuwa anatengeneza mbegu chache mno, kuna vitu vingi vinasababisha hasa matatizo ya genetics au homoni hazitoshi au viungo vyake havijakamilika,” anabainisha.
Anasema kama mtu anakabiliwa na ugonjwa wa kisukari huweza kumsababishia kushindwa kufanya vema tendo la ndoa au kupungukiwa nguvu na hivyo kushindwa kutoa mbegu au akatoa kwa kiwango cha chini.
“Au wengine wanashindwa kabisa kutoa yale majimaji kwa sababu mbegu hutoka zikiwa na majimaji yake, hali ya hewa nayo inaweza kusababisha tatizo hasa kwenye joto jingi, au kutokunywa maji ya kutosha pia ni kisababishi,” anasema.Image result for KAIRUKI HOSPITAL
Matibabu
Anasema pale wanapogundua tatizo kuna njia nyingi ambazo hutumika kuwatibu wahusika ikiwamo za kawaida na zile za upasuaji.
“Tunaweza kuwatibu kwa kuwapatia dawa maalum za vidonge wote wawili au tunafanya upasuaji wa kuzibua mirija kama imeziba au kama mayai ya mama hayakomai vizuri tunaweza kufanya upasuaji katika vifuko vya mayai yake na yakatoka yakiwa yamekomaa vizuri,” anasema.
Anasema wanaweza kufanya upasuaji huo kwa njia ya kisasa ya laparascopic na mama akaenda kuendelea na shughuli zake kama kawaida baada ya muda mfupi.
“Ikiwa njia hizo zitashindikana basi hapo tunaweza kuwafanyia njia ya upandikizaji, tunaweza kuchukua mbegu za baba na kuzitayarisha maabara huku tukisubiri mayai ya mama yakomae hapo tunachukua zile mbegu za baba na kuweka kwa mama kupitia njia ya uke.
“Njia hii imeanza kutumia tangu miakaa ya 1970 lakini ili kufanya njia hii inapaswa mirija ya mama iwe wazi (haijaziba), kama imeziba inabidi kutimia njia nyingine ikiwamo ile ya IVF.
“Mwaka 1978 alipatikana mtoto wa kwanza kwa kutumia njia hii ya IVF, baada ya hapo zikagundulika pia njia zingine ambazo zinaweza kutumika kwa wana-ndoa ambao wamekosa watoto na wakapata,” anasema.
Dk. Kairuki anasema ipo njia nyingi ambapo mbegu za baba huhifadhi na mayai ya mama hutayarishwa kwa kuchomwa sindano maalum.
“Kwa kawaida mayai mawili hukomaa kwa pamoja lakini kwa  njia hii unaweza kuvuna hata mayai 20 kwa mkupuo tunayachukua kitaalamu, tunayavuna na kuyapeleka maabara,” anasema.
IVF is the best job perk nobody talks aboutAnaongeza “Mwanaume anaweza kutoa mbegu kwa njia ya kawaida au kwa kufanya ‘masterbesheni’ tunamshauri jinsi ya kufanya au akae muda gani ili atoe.
“Ikishindikana tunampatia dawa maalum ya kumchangamsha ili zitoke zenyewe na ikiwa hazitoki kabisa tunaweza kuzichukua kitaalamu kwa upasuaji kutoka kwenye korodani zake na kuzipeleka maabara,” anabainisha.
Anasema wakizifikisha maabara huziweka pamoja na kwamba baada ya siku mbili hadi tano huwa tayari zimetengeneza ‘kijusi’ ambacho huchukuliwa na kuingizwa katika tumbo la uzazi la mama kwa njia ya uke.
“Baada ya hatua hiyo mama anapewa muda wa kupumzika labda dakika 15 kisha anakwenda zake nyumbani na ile mimba inakuwa tumboni mwake kama mimba zingine zilizopatikana kwa njia ya kawaida,” anabainisha.
Anaongeza “Tofauti yake inakuwa tu kwamba tumetayarisha maabara, kiumbe kinakuwa kikiwa maabara na tunakitumbukiza kwa njia ya uke kwenda kwenye tumbo la uzazi ambalo nalo linakuwa limeandaliwa kukipokea.
“Kwa njia ya IVF tunakuwa tumechukua mayai ya mama na kuyamwagia mbegu za baba ambazo hufuata yale mayai, kasi yake huwa kubwa zaidi kuliko njia ya kawaida kwa sababu yanakuwa yameandaliwa.
“Kwa njia ya IX tunachofanya ni kuchukua yai la mama na mbegu ya baba kisha tunachomeka moja kwa moja wakati njia ya IVF tunaingiza zile mbegu nyingi kwa pamoja,” anabainisha.
Njia mbadala
Dk. Kairuki anasema wapo wanawake ambao hawana mayai au wanayo lakini hayakidhi viwango hasa wale walio na umri mkubwa kwani yanakuwa yamepoteza ubora kwa njia hii wanaweza kupata kutoka kwa wenzao.
“Nchi za wenzetu, wana benki ya kuhifadhia mayai na mbegu za uzazi, zinahifadhiwa katika chumba chenye nyuzi joto -196 ambayo ni baridi kali sana na kuna kemikali ambazo hutumika kuhifadhia na zinaweza kukaa hata miaka 50 ndani ya chumba hicho,” anasema.
Anasema  inawezekana pia kupatikana mama ambaye yupo tayari kubeba ujauzito na baadae mtoto akizaliwa hukabidhiwa kwa wale waliochangia mbegu.
“Kwa wale ambao wana matatizo ya saratani wanaweza kutumia njia hii kwa sababu inabidi wapigwe mionzi ikiwa ni sehemu ya matibabu, inaweza kuharibu mbegu na mayai yao.
“Hivyo kabla ya kuanza matibabu hayo wanaweza kutoa mbegu na mayai yao zikahifadhiwa maabara na wakipona wanakuja kupandikiza na wanaweza kupata watoto kama kawaida,” anasema.
Ipoje kisheria
Anasema zipo sheria mbalimbali ambazo hutumika kusimamia huduma hiyo ya upandikizaji katika nchi ambazo zinafanya huduma hiyo hivi sasa duniani.
“Kunakuwa na mkataba maalum ambao husainiwa na baba na mama wa mchangiaji wa hizo mbegu ili baadae asiweze kudai mtoto wake, nchini mwetu (Tanzania) kwa sasa bado hatuna sheria.
“Kwa kuwa ni kitu kipya, nadhani Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itachukua hatua kwa kuandaa miongozo jinsi gani hili lifanyike, tutashirikiana nao ili kuhakikisha tunafuata utaratibu utakaowekwa kwa mujibu wa sheria,” anasema.
Wizara
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Mpoki Ulisubisya anasema mpango huo ni mzuri na wa kupongeza kwani utakapokamilika na kuanza utasaidia wengi.
“Nawaomba muendelee na mshikamano huo wa kubuni mambo mbalimbali yanayohusu tiba kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania, wazo hili litakapoanza litasaidia wananchi wengi.
“Hivi sasa serikali ina mambo mengi ya kufanya si vibaya watu binafsi wakiwa na miradi ambayo itaenda sambamba na msaada kwa wananchi kama huu mpango,” anasema.
Dk. Ulisubisya anaongeza “Kwa sababu ili wananchi wafanye kazi lazima wawe na afya nzuri, kuwa na afya nzuri ni pamoja na kuwa na huduma kama hizi zinazoletwa na taasisi hii, shule ipo, chuo kipo na hospitali ipo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement