Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Picha na mtandao

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam


ILI kusogeza huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo nchini, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inazidi kujikita katika utoaji mafunzo ya kibingwa dhidi ya magonjwa hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hayo juzi alipozungumza wakati wa mahojiano na Mtangazaji Hamza Kasongo katika Kituo cha televisheni, Tv E.

"Hali ilivyo sasa ni tofauti na ilivyokuwa awali tulipoanza kutoa huduma, tunaona idadi ya wagonjwa imezidi  kuongezeka na wanakuja kutoka maeneo mbalimbali nchini," alisema.
Picha na Veronica Romwald

Profesa Janabi (Pichani) alisema changamoto iliyopo hivi sasa ni uchache wa wataalamu ili kuwasambaza katika maeneo mengine kutoa huduma kwa wananchi wanaokabiliwa na magonjwa hayo.

"Kwa hiyo kwa kuanzia hivi sasa kuna madaktari watatu ambao  wanamaliza 'masters of science in Cardiology' JKCI tunawapa mafunzo kwa kushirikiana na wenzetu wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS)," alisema.

Profesa Janabi alisema huo ni mwanzo mzuri kwani baadae watapatikana wataalamu na hivyo huduma kusogezwa zaidi kwa wananchi.

Pamoja na hilo, Profesa Janabi alisema changamoto nyingine ambayo wamekuwa wakiiona ni wananchi kutokuwa na mwamko wa kupima afya zao.

"Lakini tunapokwenda kufanya 'outreach program' lengo ni kuwaona wananchi hawa hata hivyo badala ya kuja wale ambao hawajijui mwenendo wa afya zao badala yake huja wale ambao tayari wanajijua ni wagonjwa.

"Kwa mfano ilipokuja ile meli ya matibabu ya wachina hapa Dar es Salaam, wengi waliojitokeza walikuwa wagonjwa, matokeo yake mnajikuta mnageuka kuwa kliniki ya wagonjwa wakati haikuwa lengo lenu la awali," alisema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement