Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

SERIKALI imewapiga marufuku na kuwapa onyo kali madaktari wote nchini kuachana mara moja tabia ya kujaza fomu za uchunguzi bila kuwapima wananchi magonjwa husika.

Agizo hilo limetolewa mjini hapa mapema leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akitoa tamko kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani yanayofanyika Machi 24, kila mwaka.

"Ni marufuku kwa Madaktari  kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa  kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika," amesisitiza.

Ameongeza "Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya  kuanza masomo.
Waziri Ummy akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.

"Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua ugonjwa huu kila mwaka duniani, milioni moja kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15," amesema.

Amesema tafiti nyingi zinaonesha takriban  theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya ugonjwa huo na kwamba wanaishi na vimelea mwilini mwao.

"Inakadiriwa kila mwaka watu 160,000 nchini wanaugua ugonjwa huo, Kauli mbiu ya mwaka huu inasema " Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB, hivyo nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele," ametoa rai.

Waziri Ummy akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.

"Mpaka sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

"Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi.

"Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.

"Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.

"Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na  tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote nchini," amesema.

Picha zote kwa hisani ya Wizara.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement