Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdol Liberman na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliotibiwa JKCI kwa ushirikiano na Israel

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MIAKA minne ya ushirikiano wa mafunzo na matibabu dhidi ya magonjwa ya moyo kati ya madaktari bingwa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Israel yamewezesha serikali kuokoa kiasi cha zaidi ya Sh. Bilioni 70.8.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi amesema hayo leo mbele ya Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na  Waziri wa Ulinzi wa Israel,  Avigdor Liberman ambaye amefanya ziara JKCI mapema leo.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdol Liberman akiwa pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu 

"Kwa kushirikiana na Israel tumekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya kibingwa yaliyowezesha kuimarika katika utoaji huduma.

"Tunaye humu ndani Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo wa Watoto, Godwin Sharau ambaye alipata mafunzo nchini Israel ameweza kutibu wagonjwa 202 hadi sasa na bado kuna madaktari wetu saba na wauguzi watano ambao wapo nchini humo wanaendelea kujifunza," amesema
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdol Liberman akimpa zawadi mmoja wa watoto waliotibiwa JKCI kwa ushirikiano na Israel.

Awali, Waziri Ummy Mwalimu amesema wameingia makubalino kati ya JKCI na Israel ambapo wakati wowote kuanzia sasa watasaidia kuimarisha huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

"Tunawashukuru wenzetu wa Israel kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana nao ambapo wametusaidia mno na sasa JKCI imeimarika katika utoaji wa matibabu ya magonjwa ya moyo.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdol Liberman akimpa zawadi mmoja wa watoto waliotibiwa JKCI kwa ushirikiano na Israel.

"Sasa tumeingia nao mkataba wa makubalino ya kuendeleza ushirikiano ambapo madaktari wa JKCI na wa Israel watasaidia kuimarisha huduma hizi katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma," amesema.

Naye, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdol Liberman amepongeza mafanikio ambayo JKCI imepata katika utoaji huduma ya matibabu ya kibingwa dhidi ya magonjwa ya moyo nchini na kuahidi ushirikiano zaidi kati yao.

Waziri wa Ulinzi wa Israel,Avigdol Liberman, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Profesa Mohamed Janabi (mwenye suti nyeusi mbele) na badhi ya wafanyakazi JCKI wakiwa katika picha ya pamoja. 

Picha zote kwa hisani ya JKCI.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement