Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipokea ramani inayoonesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa.

NA WAMJW- KASULU KIGOMA

KIWANGO cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini kimeshuka kwa nusu zaidi  kutoka asilimia 14. 4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7. 3 mwaka 2017. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika leo Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma. 
Waziri Ummy akikagua vyandarua wakati wa maadhimisho hayo.

"Katika kuhakikisha tunatokomeza kabisa ugonjwa huo Wizara ya Afya kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tumepokea na kusambaza vitendanishi vya malaria (mRTD), vipimo 21, 428, 725, dawa za mseto dozi 12, 916, 050 kwa ajili ya maralia isiyo kali, Sindano za kutibu malaria kali vichupa 1, 668, 464 na vidonge vya SP dozi 6, 899, 700 kwa ajili ya tiba kinga dhidi ya athari za malaria wakati wa ujauzito," amesema Waziri Ummy. 
Amesema ili watanzania tuendelee kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria watanzania wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika kutumia afua zote za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kunyunyizia viuadudu vya kuua viluilui vinavyoweza kuleta malaria. 
Wananchi wakifuatilia jambo.

Amesisitiza kila wilaya kuunda kamati zitakazohamasisha usafi wa mazingira  ili kuondoa mazalia ya mbu katika kutokomeza malaria. 

Pamoja na hilo Waziri Ummy amezindua takwimu za  ugonjwa wa Malaria nchini ambao umefanywa na Taasisi ya Takwimu nchini (NBS) ambayo ndio Takwimu itayotumika na Serikali ya Tanzania. 

Naye, Waziri Wa Elimu na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema atahakikisha wanafunzi wanapambana na ugonjwa wa Malaria kwa kuweka somo la afya kwa shule zote za msingi na sekondari nchini. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emamanuel Maganga ametoa wito kwa wakazi wa kigoma kutumia vyandarua kwa matumizi sahihi na siyo kinyume na hapo ikiwemo kufungia kuku na kuvulia samaki. 
Burudani ilikuwepo 'kama kawa' uwanjani hapo

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement