NA VERONICA ROMWALD –
DAR ES SALAAM
IKIWA mtoto wako ana
tabia ya kukimbia kimbia, kuruka ruka bila kujali kwamba anaweza kuumia
kulingana na mazingira aliyopo, unapaswa kumfuatilia kwa makini.
Imeelezwa hizo ni
miongoni mwa dalili za tatizo la ajali ya ubongo ambalo linaonekana kuwakabili
watoto wengi.
Mtaalamu wa Idara ya Tiba
ya Utengamao na Mazoezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Rosemary
Kauzeni alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na MTANZANIA Jumamosi katika
mahojiano maalum.
Alisema kila siku katika
Idara hiyo hupokea watoto wapatao 20
wanaokabiliwa na tatizo hilo na watu wazima wapatao 10.
“Linawakabili pia watu
wazima lakini tunaona idadi kubwa tunaowapokea ni watoto changamoto ni kwamba
wazazi wengi hawana uwelewa kuhusu tatizo hili,” alisema.
Alisema inajulikana
wazi watoto huwa ni wachangamfu lakini inapotokea ule uchangamfu unapitilia
mzazi anapaswa kufuatilia kwa umakini.
“Uchangamfu unapopitilia si hali nzuri ni dalili za mtoto kukabiliwa na tatizo hili la ajali ya ubongo,” alisema.
Mtaalamu huyo alibainisha dalili nyingi za tatizo anazoonesha mtoto, dalili kwa watu wazima na matibabu yake.
Kujua kwa undani tafadhali usikose nakala ya gazeti la MTANZANIA alhamis wiki hii.
Chapisha Maoni