Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Image result for tezidume
Maumivu ya kiuno, mgongo ni miongoni mwa dalili za mtu mwenye tatizo la saratani ya tezidume (picha na mtandao).

NA VERONICA ROMWALD - DAR ES SALAAM

TAMKO lililotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu mpango wa kufanyika uchunguzi wa saratani ya tezidume nyumba kwa nyumba, lilibua mjadala mzito hasa mitandaoni.

Wengi wakihoji uwezekano wa kufanyika kwa jambo hili huku wengine wakidai kwamba ni suala lisilowezekana.

Kutokana na hali hiyo MATUKIO NA MAISHA hivi karibuni ilimtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dk. Julius Mwaiselage.
Image result for tezidume
Picha inaonesha tezidume iliyo salama na tezidume yenye ugonjwa (na mtandao)

Akizungumza, Dk. Mwaiselage alisema inawezekana kufanya uchunguzi wa saratani ya tezidume 'nyumba kwa nyumba'.

"Viongozi wanatoa matamko ya Sera halafu wataalamu tunapanga jinsi ya kutekeleza hiyo Sera, nadhani Sera anayotamka RC Makonda ni kwamba kila nyumba uwepo uwezekano wa kupima tezi dume".

"Na wala si wahudumu wa afya kwenda nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa kupima watu saratani ya tezidume...labda niwe sikuelewa," alisema.
Image result for ORCI TANZANIA DK. MWAISELAGE
Akitolea mfano, Dk. Mwaiselage (Pichani) alisema inawezekana kufanya uchunguzi huo kwani hata nchi za Ulaya wanafanya uchunguzi kwa kila mwananchi kwa kufuata vigezo vya saratani husika.

"Nchi za USA/Europe wana kitu kinaitwa 'targeted cancer screening for individuals at risk' yaani baada kufikia umri fulani wahusika wanaitwa kwenda vituoni kupima saratani husika.

"Tanzania tuna Mwongozo wa Taifa wa Upimaji wa Saratani Tezi dume ambapo upimaji hufanywa kupitia 'rapid PSA test' kwa kutumia damu. Upimaji huu unafanana na upimaji wa maambukizi virusi ukimwi au malaria," alisema.

Alisema majibu ya uchunguzi wa awali kwa mgonjwa husika ndiyo yataelekeza aendelee na vipimo vingine au kama ni 'negative' basi atapima baada muda gani tena kutokana na athari yake.

 "Kitu muhimu ni kuwepo na kukubali kupimwa kwa muhusika. Na pia muhimu upimaji uendane na uchaguaji wa watu kutokana na athari zao (risk profile) ili kutoku-overstretch health system," alisisitiza.
Image result for ORCI TANZANIA
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016/17 za ORCI saratani ya tezidume ni miongoni mwa saratani zenye idadi kubwa ya wagonjwa.

Takwimu hizo zinaonesha Saratani ya shingo ya kizazi inaongoza kwa asilimia 32.8, matiti asilimia 12.9, saratani ya ngozi (Kaposis Sarcoma) asilimia 11.7, kichwa  na shingo asilimia 7.6, matezi asilimia 5.5.

Saratani nyingine zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ni ya damu asilimia 4.3, kibofu cha mkojo asilimia 3.2, ngozi asilimia 2.8, macho asilimia 2.4 na tezi dume asilimia 2.3.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement