Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam

RAIS wa Chama cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA), Remla Shirim (Mwenye miwani pichani) amewahimiza wataalamu hao kujenga utamaduni wa kujiendelea kitaaluma ili kuendana na wakati hasa katika utoaji na uboreshaji huduma.

Amesema hayo leo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyoanza April 23, 2018 hadi April 25, 2018 (jana) kwa Wafiziotherapia 25, yalihusu jinsi ya kuhudumia wagonjwa waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU).
Baadhi ya Wafiziotherapia waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa umakini Rais wao (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza.

"Nawasihi mjenge tabia na utamaduni wa kurudi chuo kujiendelea kielimu ili tuendane na kasi ambayo dunia inakwenda nayo hivi sasa katika utoaji huduma za afya kwa wagonjwa," amesema.

Kwa upande wake, Katibu wa APTA ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mafunzo hayo, Abdalah Makala (anayezungumza pichani) amesema yametolewa na APTA kwa kushirikiana na wataalamu bingwa kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India.
Baadhi ya Wafiziotherapia waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa umakini Katibu wao (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza.

"Kimsingi yamelenga kuwajengea uwezo wataalamu hao wa kuhudumia wagonjwa waliolazwa ICU, kuna mabadiliko makubwa katika utoaji huduma tunahitaji kujenga uwezo wa wataalamu wetu ili waweze kuendana na kasi hiyo ya mabadiliko, na ndiyo kusudi la mafunzo haya," amesema.
Baadhi ya Wafiziotherapia waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa umakini Katibu wao (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement