Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Waziri Ummy akimuangalia mmoja wa wanafunzi akipatiwa chanjo hiyo.

*Waziri Ummy amesisitiza inatolewa bila malipo kote nchini

NA WAMJW- TANGA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watoa huduma za afya kuhakikisha wanatoa matibabu ya saratani ya mlango wa kizazi bila ya malipo yeyote kwa wananchi. 
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Pichani) wakati wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi  iliyofanyika leo Mkoani Tanga. 
Wanafunzi wakimsikiliza Waziri Ummy (hayupo pichani) 

Uchunguzi, matibabu na chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi inatolewa bila ya malipo yeyote katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zinazomilikiwa na Serikali" amesema Waziri Ummy. 
Wananchi wakimsikiliza Waziri Ummy (hayupo pichani) 

Amesema ni lazima wazazi au walezi wa watoto wanaopata chanjo waridhie ili kuweza kuwapa chanjo hiyo kwani kinga ni bora kuliko tiba. 

Naye, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Tanga Dk. Malisely amesema lengo la Mkoa wa Tanga ni kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wapatao 38, 000 mkoani humo. 
Burudani...

Dk. Malisely amesema ni lazima tuwaelimishe na tuwaeleze wazazi umuhimu wa mtoto kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kujikinga na ugonjwa huo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Bw. Thobias Mwilakwa amehimiza wazazi na walezi mkoani humo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata huduma ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement