Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
NA VERONICA ROMWALD - DAR ES SALAAM

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa dawa na vifaa tiba zaidi ya 2,000 vitakavyotumika kufanikisha upasuaji kwa wagonjwa wenye tatizo la mtoto wa jicho. 

Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida amemkabidhi vifaa hivyo jana Mei 28, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk. Julieth Magandi.

Akizungumza, Balozi Yoshida amesema hatua hiyo ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Japan na Muhimbili wa zaidi ya miaka 11 sasa.

Naye, Dk Magandi ammshukuru Balozi Yoshida kwa kuendeleza uhusiano mwema na ushirikiano walionao. 

Awali akizungumza,  Yamasaki amesema mtoto wa jicho ni tatizo linalokabili watu wengi hasa wenye umri wa utu uzima duniani na kwamba ikiwa hawatapa matibabu huwa kwenye hatari ya kupata upofu. 

Naye, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho wa Muhimbili, Neema Kanyaro amesema huwa wanahudumia wagonjwa wapatao 10 hadi 20 kila siku kliniki hasa watu wazima. 

Amesema kambi hiyo ya matibabu itadumu kwa siku tatu kuanzia Mei 28 (leo)  hadi 30, mwaka huu.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement