Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MAZOEZI ni muhimu kwa afya ya mwanadamu lakini ikiwa yatafanyika kiholela muhusika anajiweka katika hatari zaidi kuathirika afya yake badala ya kupata faida, imeelezwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema hayo katika mahojiano haya maalum.

Amesema kufanya mazoezi pasipo kuchunguzwa kwanza afya ni hatari kwani ikiwa mtu anakabiliwa na magojwa mbalimbali hasa ya moyo anaweza kuanguka na kufariki dunia ghafla.

“Ninapoona ‘wimbi’ la 'gym' kila mahala huwa ninatafakari, je wale wanaokwenda huko kufanya mazoezi wamechunguzwa afya zao na nani? Nakumbuka katika gym (anaitaja) ni kubwa hapa Dar es Salaam, kuna mtu alianguka, wakati akifanya mazoezi.

“Sasa, hiyo ni 'gym' kubwa na mtu alianguka, jiulize wangapi wanakwenda huko hawajijui afya zao, ni hatari kama mtu ana shinikizo la damu anaweza kujipata akianguka ghafla na kupoteza maisha au hata kupata kiharusi,” amesema.

Amefafanua “Kimsingi kadiri mtu anavyofanya mazoezi ndivyo mahitaji ya damu mwilini mwake yanavyoongezeka, tunashauri mtu asifanye mazoezi aina yoyote hasa yale magumu na ya muda mrefu bila kuchunguza afya yake kwanza.

“Katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika Septemba 26, mwaka huu hapa JKCI tulitangaza upimaji afya bila malipo.

“Walijitokeza watu 801 kupima afya, watu 400 kati yao walikutwa wana shinikizo la juu la damu, 200 kati yao walikuwa hawajijui na kati ya 150 hadi 200 walikuwa wanajijua lakini walikuwa hawatumii dawa vile inavyopaswa na hivyo kuhatarisha maisha yao zaidi,” amesema.

Mahojiano haya kwa kina yanapatikana katika makala yenye kichwa cha habari 'MSHTUKO WA MOYO MICHEZONI YAZINGATIWE HAYA KUOKOA MAISHA'. Hapa hapa MATUKIO NA MAISHA BLOG

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement