Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Mary Haule, akiuliza swali wakati wa   kikao cha nne cha  Baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo  kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.

Na Veronica Mrema – Dar es Salaam

Uongozi wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umejivunia baraza hilo kuwa huru kwa wajumbe kuwasilisha maoni yao na kufanyiwa kazi kama ilivyokusudiwa na uongozi sikivu wa menejimenti ya taasisi hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Mohamed Janabi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika Protea Hotel jijini hapa, Katibu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE – JKCI), Joyce Mugala amesema limekuwa lenye mafanikio makubwa.

“Tumeona Mkurugenzi Mtendaji amekuwa akipokea na kufanya yale tunayojadili na kutupa mrejesho kwa wakati, limekuwa baraza sikivu kwani menejimenti imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na wafanyakazi hususan kwa upande wa maslahi,” amesema.

Joyce ameongeza “Kama mnavyojua mgogoro mkubwa wa wafanyakazi ni maslahi na uongozi, lakini tunashukuru Mkurugenzi Mtendaji wetu amekuwa msikivu anatupa kile tunachowasilisha kwa mfano posho kwa wafanyakazi tuliomba kwenye kikao alilichukua na tukapewa,” ametoa mfano.

Joyce ameongeza “Sisi wafanyakazi tunajivunia limekuwa Baraza 'productive' maana yale tunayoshauriana na uongozi yanatendewa kazi.

“Vitendea kazi JKCI is perfect hatuna tatizo lolote kwa upande huo, kuanzia mazingira ya ofisi, utendaji 'theater' na 'cathlab' watu wapo 'happy', kutokana na mazingira ya ofisi na vitendea kazi.

“Menejimenti imejali mpaka kufikia hatua ya kuongeza 'cathlab' nyingine, tunashukuru pale tunapohitaji kitu, inasikia na kuyafanyia kazi, hii ni maabara ambayo mtaalamu anaweza kuuchunguza moyo ulivyo na kuweza kutibu inapohitajika.

“Furaha ya Watanzania ni pale JKCI inapotoa huduma bora na nzuri kwao, tunakwenda kutoa huduma Bora zaidi,” amesisitiza Joyce. 

Naye, Ofisa Ugavi Msaidizi wa JCKI, Rajabu Nasibu amesema kwa upande wa manunuzi kumekuwa na mafanikio Taasisi imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Tulipoanza ilikuwa Taasisi changa mwendo wake ulikuwa ukisuasua, hatukuwa na vifaa kama tulivyonavyo sasa, tumepiga hatua, malengo yanaongezeka hata kwa upande wa manunuzi ya vifaa tiba awali watu binafsi ndiyo walikuwa wanavileta nchini sasa hivi Serikali ndiyo inayoagiza na kuleta moja kwa moja nchini,” amesema.

Prof. Janabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema limekuwa kiunganishi kikubwa kati ya wananchi, wafanyakazi na menejimenti ya Taasisi hiyo.

“Tunajivunia utulivu mkubwa uliopo kwenye Baraza hili, menejimenti inaongoza wafanyakazi 310 na wote wanahitaji kupata huduma wanazostahili ili wananchi wapate huduma ambazo nchi inafikiria kuzitoa kwao,” amesema.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Mtaki akitoa mada ya sheria za kazi  kwa wajumbe wa kikao cha nne cha  baraza la wafanyakazi wa   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Roberth Luchemba  akichangia mada ya sheria za kazi wakati wa kikao cha nne cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wajumbe 59 walihudhuria kikao hicho.  

Picha na JKCI

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement