Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Wetu 

Waandishi wa habari wawili wa Tanzania wametajwa miongoni mwa washindi waliotwaa tuzo Barani Afrika inayoangazia Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID – 19) zinazotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Merck Foundation lenye makao yake makuu nchini Ujerumani.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk. Rasha Kejel, imewataja Watanzania hao ni Mwandishi wa kujitolea wa Habari za Afya na za Kijamii Veronica Mrema ambaye aliposhiriki tuzo hizo alikuwa akichangia katika gazeti la JAMVI LA HABARI linalochapishwa na kampuni ya Ador Tanzania Limited, mwandishi mwenzake aliyetajwa ni Mwanaisha Makumbuli wa Highlands FM Radio.

"Pongezi nyingi kwa washindi wa tuzo 'stay at home' kwa mwaka 2020 kutoka Ukanda wa Mashariki mwa Bara la Afrika, ambao mmechaguliwa kuwa washindi, tulipata mwamko mkubwa wa washiriki, leo najivunia kutaja orodha hii ya washindi katika vipengele vinne," amesema Dk. Kejel.

Pamoja na Watanzania hao, waandishi wengine katika Ukanda huo wa Afrika Mashariki wanatoka nchini Kenya, Rwanda  na Uganda.

Pamoja na washindi wa Ukanda wa Afrika Mashariki shirika hilo pia limewatambulisha washindi kutoka wa Ukanda wa Magharibi mwa Afrika, wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa, nchi zinazozungumza lugha ya kireno na wa ukanda wa kusini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa Merck Foundation tuzo hiyo ilikuwa ikiangazia namna ambavyo waandishi wa habari barani humo walivyoweza kusaidia jamii zao kufikisha taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini China, Desemba mwaka jana unaosababishwa na maambukizi ya vizuri vya Corona.

Dk. Kejel ametaja majina ya washindi hao na vipengele walivyoshinda kama ifuatavyo;

*ONLINE CATEGORY WINNERS*

FIRST Position: 

- *_Hillary Orinde_* - Standard Media Group, *KENYA*

 SECOND Position:

- *_Arnold Kwizera_* - CNBC Africa, *RWANDA* 

 THIRD Position:

- *_Geoffrey Kamadi_* - Scientific African, KENYA 

 *PRINT CATEGORY WINNERS*

 FIRST Position: 

- *_Esther Oluka_* - Daily Monitor, *UGANDA* 

 SECOND Position:

- *_Veronica Romwald Mrema_* - Jamvi La Habari, *TANZANIA* 

- *_Lydia Atieno Barasa_* - The New Times, *RWANDA* 

 THIRD Position:

- *_Evelyn Makena Gatobu_* - People Daily, *KENYA* 

 *MULTIMEDIA CATEGORY WINNERS*

 FIRST Position: 

- *_Mashirima Kapombe_* - Citizen TV, *KENYA* 

- *_Dorcas Wangira_* - Citizen TV, *KENYA* 

 SECOND Position:

- *_Daniel Sebakijje_* - NBS TV, *UGANDA* 

*RADIO CATEGORY WINNERS*

FIRST Position: 

- *_Mwanaisha Makumbuli_* - Highlands FM Radio, *TANZANIA* 

 SECOND Position:

- *_Kigongo Issa_* - Radio Bilal, *UGANDA* 

We will do a video conference meeting with all the winners together soon.

Dk. Rasha Kejel,

CEO of Merck Foundation.

1 Maoni

  1. Hongera kwa washindi wa Tanzania kwa kututoa kimasomaso. Endelezeni kasi hiyo hiyo

    JibuFuta

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement