Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na WAMJW – Dar Es Salaam

Wauguzi na wakunga nchini wamekumbushwa kuhakikisha wanatunza vizuri taarifa za kazi kwenye majarada ya kazini kwa kuandika yale yote ambayo wanafanya tangu wanapoingia kazini hadi kutoka.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ziada Sellah alipokuwa akizungumza na wauguzi na wakunga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala – Dar Es Salaam.

“Kila unachofanya kazini aidha umemhudumia mgonjwa au ukiwa na majukumu mengine hakikisheni mnatunza taarifa za kazi kwa kuandika kwenye majadara yenu ya kazi” amesema Bi. Ziada.

Bi. Ziada amesema kuwa kwa kufanya hivyo itawasaidia pia madaktari, wauguzi na wakunga wengine wanaoingia zamu tofauti kutambua kwa haraka nini ambacho kimefanyika na kuweza kuendelea na kazi ambayo wengine wameacha. 

Amesema kuwa wauguzi na wakunga wamekuwa wakilaumiwa kwa kutotunza vizuri taarifa za utendaji kazi jambo ambali hupelekea changamtoto kwa wagonjwa kutopata huduma sahihi wakiwa hospitalini.

“Tumekuwa tukilaumiwa hatutunzi kumbukumbu zetu vizuri, andikeni kila mnachofanya, kama umemwita daktari saa 1, hadi saa 3 hajafika andikeni, tufanye ‘documentation’ kadiri inavyowezekana” amesisitiza Bi. Ziada.

Hata hivyo Bi. Ziada Sellah hakusita kuwakumbusha wauguzi na wakunga kufanya kazi kwa malengo ili waweze kujipima ufanisi wa kazi zao na kujua eneo wanapofanya vizuri na kwenye changamoto.

“Tufanye kazi kwa malengo ili mwisho wa siku tuweze kujipima kwa kufanya tathimini ya malengo tuliyojiwekea kubaini kama tumeweza kuyatimiza” amesema Bi. Ziada.

Amesema kuwa malengo yanaweza kuwa ya siku moja hadi mwaka mmoja kulingana shabaha ulizojiwekea muuguzi au mkunga na yatawaongoza kujua ni wapi walikwama na wapi walifanikiwa.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Bi. Ziada Sellah akisema jambo kww wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Dar es Salaam (hawapo pichani).
Picha ya Pamoja Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Bi. Ziada Sellah pamoja na Wauguzi na Wakunga Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Mwananyamala, Dar es Salaam.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement