Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

"Ajali za barabarani katika msimu wa sikukuu zinaweza kuchangia ongezeko la uhitaji wa damu, hivyo ni muhimu kuzingatia alama za barabarani, kuepuka ajali," anasema Dk. Liymo. 

Na Veronica Mrema – Dar es Salaam

Watanzania wamehimizwa kuepuka ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu kwani endapo hawatazingatia, ajali zinaweza kusababisha changamoto ya uhitaji wa damu kuongezeka.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS), Dk. Magdalena Liymo alipozungumza na MATUKIO NA MAISHA BLOG katika mahojiano maalu, hivi karibuni.

Dk. Liymo amesema katika kipindi cha msimu wa sikukuu tathmini zinaonesha huwa kunatokea matukio ya ajali za barabarani kama siku za hivi karibuni ndiyo maana anatoa rai hiyo kwa Watanzania.

“Tupo katika msimu wa sikukuu ya krismasi kuelekea sikukuu ya mwaka mpya, ni kipindi ambacho shule nyingi huwa zimefungwa, NBTS huwa tunakusanya damu kutoka kwa wachangiaji walioko mashuleni, ndiyo maana katika kipindi hiki huwa tuna kampeni maalum tumeipa jina ‘Toa Zawadi ya Uhai kwa Mwenzako’, tukihamasisha jamii kujenga utamaduni wa kuchangia damu.

“Katika msimu wa sikukuu, wanaosafiri barabarani ni wengi, kwa msingi huo tunahamasisha wanasafiri kuwa makini barabarani hasa madereva, kwa sababu ni kipindi ambacho huwa tunashuhudia ajali zikitokea mara kwa mara.

“Kutokana na ajali hizo wakati mwingine huweza kuchangia kuongezeka kwa mahitaji ya damu nchini, katika kipindi hicho cha sikukuu, tunawasihi Watanzania wajiangalie huko barabarani, wawe salama, wawe makini tupunguze ajali,” amesisitiza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement