Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Waziri Gwajima akimsikiliza mmoja wa wataalamu ambao tayari wamepatiwa mafunzo kuanzisha huduma hiyo nchini.

Na Veronica Mrema – Dar es Salaam

Mfumo wa kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto (ute wa mifupa) kwa wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo ya damu kama vile saratani, siko seli na mengineyo, upo hatua za mwishoni kukamilishwa, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Huduma hiyo inatarajiwa kuanza mara moja baada ya kuwasili na kufungwa kwa kifaa kimoja tu kilichosalia kukamilisha mfumo, kilichoagizwa kutoka China ambacho hivi sasa kipo njiani kuja nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili (Upanga na Mloganzila), Profesa Lawrence Museru, amemueleza hayo leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima alipofanya ziara katika hospitali hiyo.

Prof. Museru amesema kifaa hicho kitakapowasili na kufungwa mfumo utakuwa umekamilika na wapo tayari kuanza kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji, ifikapo Machi, 2021.

“Huduma hii itatolewa na hospitali zetu zote mbili (Muhimbili upanga na Mloganzila), wagonjwa watakuwa wakilazwa kule Mloganzila na seli zitakuwa zinachukuliwa na kuhifadhiwa hapa Upanga kwenye mashine tulizonazo,” amebainisha.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu Muhimbili, Stella Rwezaula amesema wataalamu tayari wapo kamili kwani walishapelekwa nje ya nchi kupata mafunzo jinsi ya kukamilisha utoaji wa huduma hiyo.

“Mashine iliyopo njiani kuja nchini ni muhimu yenyewe ipo kama ile mashine ya dialysis (uchujaji damu kwa wagonjwa wa figo), ambayo itatuwezesha kuvuna zile seli kutoka kwa (donor) mchangiaji ambapo pia wachangiaji wataweza kuchangia mara nyingi,” amebainisha.

Akizungumza, Waziri Gwajima amewapongeza Muhimbili kwa kufanikisha hatua zote za msingi kuelekea uanzishwaji wa huduma hiyo ili kutimiza adhima ya serikali kuendelea kuboresha huduma za kibingwa nchini.

“Muhimbili na wataalamu wote wa hospitali nyingine zinazotoa huduma za kibingwa na ubingwa wa juu wamefanya zimefanya kazi nzuri, natambua mchango wao mkubwa katika kuboresha huduma za afya nchini.

“Kwa miaka mitano iliyopita wameokoa fedha nyingi kutokana na huduma zilizoanzishwa chini ya Rais. Dk. John Magufuli, ambaye alipoingia tu alianza na muhimbili na ndipo alianza adhima yake ya kuboresha huduma za afya, imesaidia kuimarisha vituo vya afya kjatika ngazi za msingi. 

“Nilifika hapa nikitaka kujua, wanandeleaje katika miaka mitano ijayo, watanipa andiko zima la mwelekeo wao na kuna maeneo wameanza kuyafanyia kazi.

Ameongeza “Nimeona upandikizaji wa uloto wa mifupa, tulikuwa tunapeleka nje ya nchi wakafanyiwe upandikizi wa chembe chembe hai, wameshajiandaa chmba, vifaa na watu wameshapewa ujuzi wauguzi na madaktari.

“Isipokuwa hiyo mashine ambayo ipo njiani hivi sasa ambayo itakuwa inatumika kuzalisha mahitaji ya damu kwa sababu watakuwa wanahitaji damu nyingi, tunawaombea ifikapo Machi, 2021 ianze mara moja,” amesisitiza.

Waziri Gwajima amesema Muhimbili pia ipo katika hatua nzuri kuanzisha huduma ya matibabu kwa kundi la wagonjwa ambao watahitaji ‘first track services’.

“Hawa ni wagonjwa wanaohitaji kulipia huduma lakini kwa kuwa hatuna huwa wanalazimika kwenda hospitali nyingine binafsi ambako wapo wanaosema huko gharama ni kubwa na wengine huenda kuzifuata hata nje ya nchi.

“Tunajaribu kuja na ‘parkage’ ya huduma ambayo itawafaa watu mbalimbali kama wanavyofanya nchi zinazoendelea, Suma JKT, wameanza awamu ya kwanza ya ujenzi ngazi ya msingi, kufikia Februari 2021 wataanza kulinyanyua jengo hili kwenda juu,” amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement