Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema – Aliyekuwa Dodoma 

Wagonjwa wa saratani wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), wameanza kupatiwa majibu ya vipimo vya sampuli zao ndani ya siku moja hadi mbili, badala ya wiki mbili hadi mwezi ilivyokuwa hapo kabla ya kuimaishwa kwa kitengo cha uchunguzi vimelea vya magonjwa hasa ya saratani (Pathology).

Kabla ya kuimarishwa kwa Idara ya pathology ndani ya maabara ya hospitali hiyo, wataalamu walilazimika kusafirisha sampuli za wagonjwa jijini Dar es Salaam (Hospitali ya Taifa Muhimbili) ambako ilichukua wastani wa mwezi mmoja kurudishwa.

Yalibainishwa hayo hivi karibuni na Afisa Mteknolojia Maabara (Histotechnologist), Michael Mazoya alipozungumza na MATUKIO NA MAISHA BLOG katika mahojiano maalum kuhusu huduma za uchunguzi wa magonjwa ya saratani zinazofanyika hospitalini hapo.

“Tunajihusisha na uchunguzi wa vimelea vya saratani ndani ya maabara, kabla ya kuanza huduma hospitalini hapa, ilitulazimu kukusanya sampuli za wagonjwa na kuzituma Dar es Salaam.

“Wagonjwa walilazimika kusubiri hadi yarudishwe ndiyo waelezwe kilichobainika, lakini kuanzia Oktoba 5, 2020 idara hii ilipoanza kutoa huduma, tulianza na wagonjwa 31 ambao sampuli zao zilitumwa (zililetwa) hapa BMH.

“Tangu hapo, wagonjwa wa saratani uchunguzi wao tumekuwa tukiufanya hapa sisi wenyewe, imemsaidia mgonjwa kwa sababu mwanzoni alikuwa anapata shida kusubiri majibu ndani ya wiki mbili hadi mwezi mzima.

“Lakini sasa anapata majibu ndani ya siku moja hadi mbili, tunatumia vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa juu kufanya sampuli nyingi kwa wakati mfupi.

“Hatufanyi ‘manual’ sana, tunatumia vifaa vyote vya kisasa, vyenye uwezo wa juu kufanya sampuli nyingi kwa wakati mfupi, inaturahisishia katika utendaji kazi, ni mazingira rafiki hatuhangaiki katika utendaji kazi wa moja kwa moja,” alisisitiza.

Afisa Mteknolojia huyo aliongeza “Katika utoaji wa huduma, zipo aina tatu, kwanza ni ile ya tissue ambayo mtaani wamezoea kuita kipimo cha kinyama, tunafa ya uchunguzi wa kubaini vimelea hasa vya saratani, zipo pia vimbe ambazo si za saratani, tunazibaini pia.

“Tuna mashine moja ambayo sijawahi kuiona sehemu nyingine nchini, inatupa uwanja mpana wataalamu, kuweza kuchunguza na kubaini vimelea vya saratani, katika hali kwamba,… daktari anakuwa anaendelea na ‘procedure’ wodini.

“Tunachukua sehemu ya ule mpaka ambapo mgonjwa alikatwa (tunaita margin’ kitaalamu) kisha tunakwenda kukichunguza kujua iwapo saratani inaendelea au amekwisha kupona,” alisema.

Alifafanua “Katika matibabu ya saratani kuna ambazo ukitoa kinyama inakuwa tayari umetibu, nyingine zinakuwa tayari zimesambaa mwilini tunakuja kufanya ‘grading’ ili tujue mtu anastahili dozi kiasi gani, kama ni kwa dawa au mionzi na wakati mwingine mazoezi kulingana na hali aliyonayo mgonjwa.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement