Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement
Baadhi ya watoto wenye magonjwa ya saratani wanaotibiwa Muhimbili, wakimuimbia wimbo Waziri Gwajima alipowatembelea mapema hii leo.

Na Veronica Mrema – Dar es  Salaam 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imeeleza namna ambavyo kitengo cha Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS), Kanda ya Kusini, kinavyosaidiana nacho katika upatikanaji wa damu salama.

Mtaalamu wa Maabara wa Muhimbili, John Bigambalayo amemueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima wakati wa ziara yake mapema hii leo kwenye kitengo hicho kwamba kwa upande wa Dar es Salaam, huwa wanapata kiwango kidogo cha damu salama pale wanapohitaji.

“Muhimbili tunajitegemea damu salama kwa asilimia 80, tunapokusanya damu kutoka kwa ndugu wa wagonjwa na wachangiaji wengine wanaokuja moja kwa moja kwenye kitengo chetu huwa tunapata chupa za damu kati ya 30 hadi 50.

“Tunapokwenda nje kuwafuata wananchi (outreach) ili wachangie huduma huwa tunapata kati ya chupa za damu 60 hadi 70 na wakati mwingine 30.

“Kuna wakati tunapoomba NBTS kwa mfano chupa 50 unakuta tunapata mbili hadi tano, kwa Dar es Salaam ni changamoto lakini kwa NBTS Mtwara  huwa tunapata chupa nyingi za damu, kwa mfano haa 100, wanatupatia,” amebainisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amemueleza Waziri Gwajima kwamba sera inabainisha NBTS ina wajibu wa kuipatia Muhimbili chupa za damu pale inapohitaji.

“Tunaomba NBTS iimarishwe ili iweze kutimiza jukumu lake ipasavyo,” amesema.

Waziri Gwajima ameipongeza Muhimbili kwa kuimairisha kitengo hicho na kushirikiana na kusisitiza kwamba atafuatilia kwa ukaribu suala hilo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement