Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Waziri Jafo akimkabidhi cheti Mwakilishi kutoka Chama cha Walimu Tanzania kwa kushiriki bega kwa bega na Global Education Link katika kuandaa mkutano huo.

Na Veronica Mrema – Dodoma

Wakurugenzi wa Halmashauri waliowanyima vibali walimu wakuu wa shule za sekondari, kuhudhuria mkutano wa mwaka uliofanyika kwa siku tatu, jijini hapa, wametakiwa kujieleza.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo juzi alipokuwa akifungua mkutano huo Desemba 20, mwaka huu.

Waziri Jafo alitaja halmashauri ambazo wakurugenzi wake wanapaswa kuandika barua ya kujieleza ni Msalala, Kahama DC, Korogwe DC na Sikonge.

“Wakurugenzi hawa hawajatoa kibali kwa walimu wakuu wake kuhudhuria mkutano huu ambao ni wa muhimu kujadili kuhusu elimu, nawataka waandike maelezo kwanini hawakutoa vibali na Katibu Mkuu wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu alisimamie jambo hili, nitalifuatilia,” alisema.

Waziri Jafo alisisitiza walimu ni watu wa mapinduzi, wanafanya kazi kubwa katika kusimamia elimu nchini na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli inawaamini.

“Tutaendelea kuweka mazingira wezeshi katika elimu kwa walimu ili waendelee kufundisha vizuri na kwa wanafunzi pia waweze kujifunza vizuri,” alisema.

Alisema katika mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imekusudia kuhakikisha shule zote za sekondari zinakuwa na maabara kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo.

Waziri Jafo akiwa katika banda la benki ya NBC kwenye viwanja vya ukumbi wa CCM ambako mkutano huo ulifanyika.


Waziri Jafo akiwa katika picha ya pamoja na walimu wakuu waliohudhuria mkutano huo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement