Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum - Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu hii leo amefanya ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha.

Waziri Ummy amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu ya Zanzibar (pichani).

 Katika mazungumzo yao Mhe. Mwalimu amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais- Zanzibar ameridhia kuendeleza jitihada za kutatua changamoto za Muungano zilizobakia.

"Mhe. Rais nikuhakikishie kwa nitafanya kazi kwa karibu sana na Mhe. Khalid Waziri mwenzangu kuhakikisha hoja ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi zinafanyiwa kazi na mwanzoni mwa mwezi Januari tunategemea kuwa na kikao cha pamoja baina yetu" Alisisitiza Mhe. Ummy.

Kwa upande mwingine Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza kwa kuteuliwa tena kuwa Waziri na kusisitiza kuwa Serikali yake itampa ushirikiano katika kuratibu masuala ya Muungano.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad (pichani), Chukwani Zanzibar.

Mhe. Hamad amesisitza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutatana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement