Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Maabara ya Taifa imeondolewa katika orodha ya chaguo (option) la vituo vya kutolea sampuli za kupima COVID -19 kwa njia ya RT - PCR kwa wasafiri katika mfumo wa kutuma miadi wa pimacovid.moh.go.tz.

Kwa mabadiliko hayo, kuanzia Machi Mosi, 2021, wasafiri wote wanaohitaji kipimo hiki wanaelekezwa kupata huduma ya kuchukulia sampuli katika Vituo / hospitali za Mjini Dar es Salaam na Mikoani kote (ona kiambatanisho) na baadae kutumiwa vyeti kwa njia ya mfumo wa TEHAMA. 

Maelekezo hayo yametolewa leo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tangazo lililosainiwa na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya), Gerard Chami.

Chami amesisitiza haitaruhusiwa tena  wasafiri  kwenda moja kwa moja Maabara Kuu iliyoko Mabibo Dar es Salaam, kwa ajili ya kipimo au majibu/vyeti.

"Lengo ni kuongeza ufanisi wa majibu na kuondoa mrundikano wa wasafiri katika maabara kuu," amebainisha.

Ameongeza "Maabara ya Taifa imekuwa ikichukua sampuli, ikizichakata, kuzipima, kutoa majibu pamoja na kuandaa vyeti kwa wasafiri. 

"Aidha, katika kutekeleza jukumu hilo, kumekua na wasafiri wengi wanaofika kwenye Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo la maabara. 

Kwa mabadiliko mapya, Chami amesema wasafiri wanakumbushwa tena kuchukuliwa sampuli siku tatu (masaa 72) kabla ya kusafiri ili kuepuka kuchelewa kwa vyeti.

"Aidha, utaratibu wa kupima sampuli kwa kipimo cha haraka cha protini za kinga (COVID-19 IgM Antibody Testing) utaendelea kufanyika katika Maabara hii ya Taifa (kwa wasafiri maalumu tu) kwa utaratibu uliokuwepo wa kufika Maabara ya Taifa kuchukuliwa sampuli na kupata cheti cha kipimo hiki kwa wasafiri wanaohitaji kipimo hicho kulingana na mahitaji ya nchi husika wanazokwenda kama China, Korea, etc.

"Vile vile kwa wasafiri maalumu wale wanaohitaji kipimo cha haraka cha COVID-19 Antigen wataendelea kupimwa katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere International Airport (JNIA) na Kilimanjaro International Airport (KIA) yakiwa ni matakwa ya ndege zao ambapo watapimwa saa nne kabla ya ndege kuondoka. 

"Wasafiri wote watatakiwa kwenda kwenye vituo vya kuchukulia sampuli kama ilivyotolewa kwenye Mwongozo wa Ushauri kwa Wasafiri (Travellers Advisory). 

"Hivyo kuanzia tarehe 01 Machi, 2021 Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii haitapokea wasafiri na kuwachukua sampuli na badala yake itabaki na jukumu la kupiman kutoa vyeti ikiwa ndio jukumu lake la msingi," amesisitiza Chami. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement