Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema 

Elimu inayotolewa na wataalamu wa afya, kuimarisha usafi, kujifukiza, kufanya mazoezi, kula lishe bora, kunywa maji mengi bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo Taifa hili limejaaliwa, ni mambo ambayo Watanzania wamehimizwa kuyazingatia ili kuzidi kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya CORONA.

Virusi hivyo ndivyo vinavyosababisha Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID 19), ambapo hivi sasa kuna wimbi la pili ambalo bado linaitesa dunia huku kukienea taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili katika nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesisitiza Wizara yake haina mpango wa kupokea Chanjo ya COVID-19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye mataifa mengine

Waziri huyo amesisitiza "Serikali kupitia wizara ya afya inazo taratibu zake za kufuata pale inapotokea kupokea bidhaa yeyote ya afya na hufanyika baada ya Serikali kujiridhisha na si vinginevyo.

Dk. Gwajima ametoa ufafanuzi huo kufuatia maswali ya wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza.

Ameagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya, wafawidhi na maafisa afya mazingira nchini kuendelea kuimarisha mifumo yote ya udhibiti na kinga ya magonjwa kwa kushirikiana na wananchi ili kudhibiti magonjwa  yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Amesisitiza Serikali itaendelea kuchukua tahadhari zote za ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa yote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote na kuendelea kuelimisha wananchi juu ya hatua za kuchukua.

Sambamba na hilo, Dk. Gwajima amesema Wizara kwa kushirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Tiba Asili na wananchi wajuzi wa tiba asili tayari wameshafanya usajili wa bidhaa (dawa) za tiba asili, alizitaja miongoni mwa dawa hizo ni COVIDAL, NIMECAF, PLANET++, BINGWA na COVOTANXA.

Ameongeza bidhaa za mafuta tete ambayo imehakikiwa na Mkemia Mkuu kuwa ni salama na zinatumiwa na watu mbalimbali ni Uzima Herbal Drops, BUPIJI, EUCALYPTUS OIL, LEMONGRASS ESSENTIAL OIL na bidhaa zingine zitaendelea kutajwa na Baraza la Tiba Asili

“Uko ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu watu wengi ambao wamepata nafuu na kupona  magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ambukiza yaliyokuwa yanawasumbua mara baada ya kutumia dawa za tiba asili hata kama walikuwa kwenye matibabu mengine ya dawa za hospitali," amesema Dk. Gwajima.

Amelielekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoa orodha ya dawa zote ambazo zimepita kwenye utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kimaabara, Maabara  ya Mkemia Mkuu wa Serikali na matokeo ya awali ya uchunguzi kuonesha ni salama kwa matumizi na kuwa dawa hizo zimekuwa zikitumiwa  na watu wengi kwa muda mrefu na kuwaponya ama kupata nafuu.

Dk. Gwajima amewataka wataalamu wote na wajuzi wa tiba asili wasisite kujitokeza na kufuata taratibu za kuwasilisha dawa  na bidhaa zao kwa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali  ili zifanyiwe uchunguzi wa kimaabara  kabla ya kukabidhi taarifa ya matokeo ya uchunguzi  Baraza la Tiba Asili  na Tiba Mbadala.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imeboresha kwenye viwanja vya ndege, mipaka pamoja na sehemu za kupimia magonjwa mbalimbali ili yasiingie nchini kwa watu wanavyoingia na kutoka.

Dk. Mollel amewataka wataalamu wa afya kuacha kufikiria mgonjwa anavyoenda kwenye kituo cha afya anaumwa kifua ana Corona bali kuhakikisha wanampima vipimo vingine ili wasije kuuwa watu na mambo mengine ambayo hayana uhusiano na Corona.

1 Maoni

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement