Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum 

Dawa za Serikali aina saba (7) zenye thamani ya sh. 265,000 zimekutwa katika duka la dawa muhimu liitwalo ROGECHU, kijiji cha Mpendoo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Kanda ya kati.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na  Meneja Mahusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Gaudensia Simwanza amesema
dawa hizo zimekamatwa ndani ya duka hilo Machi 2, 2021.

"Mamlaka ilifanya ukaguzi katika maeneo yanayojishughulisha na biashara ya dawa na vifaa tiba katika kijiji hicho na kukamata dawa hizo kwenye duka hilo," amesema.

Amesema mtuhumiwa (anayeonekana pichani) amekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Chemba, Kanda ya Kati ambako bado anashikiliwa, taratibu nyingine za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zinaendelea.

2 Maoni

  1. Ongereni kwa kazi nzuri mnayofanya

    JibuFuta
  2. Ongereni sana kwa kazi nzuri mliyofanya chemba

    JibuFuta

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement