Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum

Bodi za wadhamini katika sekta ya afya zimeagizwa kuwa karibu na watumishi kuwasikiliza kero na malalamiko yao na si kusubiri vikao vya bodi peke yake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia masuala ya afya, Prof. Abel Makubi ameagiza hayo alipozungumza na waandishi wa habari.

Prof. Makubi alikuwa akizungumzia mambo mbalimbali yatayotekelezwa na Wizara hiyo katika  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika Juni 18, hadi 23, mwaka huu.

"Bodi zisisubiri vikao vya bodi peke yake, wajumbe wa bodi waende kuonana na watumishi... kuna mambo watumishi wanaweza wasiieleze Menejimenti wakajieleza kwa mwenyekiti wa bodi," amesema.

Ameongeza "Menejimenti za hospitali kwa kushirikiana na kamati za afya ambazo zipo kuanzia ngazi za vijiji, mtaa, halmashauri na hospitali za Kanda na zile za rufaa za mikoa watembelee wagonjwa kuwajulia hali na kuwasilikiza kero zao.

"Watoe elimu kwa wananchi kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ya kuambukiza.

"Tumekuwa (Wizara) tunaelimisha jamii kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na ya kuambukiza, 'spirit' hiyo ishuke mpaka kule chini," ameagiza.

Sambamba na hilo, Prof. Makubi amesema katika wiki ya kwanza ya Julai, mwaka huu, Wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, wamepanga kupokea kero, malalamiko na maoni kutoka kwa wananchi.

"Maandalizi yanaendelea, tutakuwa na namba maalum za simu za kupiga, so makao makuu tu, hadi kwenye vituo vyote (taasisi za afya) na tumeshatoa namba maalum kwa ajili ya 'magrupu maalum ya 'whatsApp' kwa ajili ya kupokea kero, malalamiko na maoni kutoka kwa wananchi," amebainisha.

Ameongeza "Tutumie lugha nzuri kuwapokea, kuwahudumia wananchi, sekta nzima tumejipanga.

1 Maoni

  1. Habari Nawapongeza sana Wizara ya afya kwa juhudi kubwa mnazofanya kubiresha huduma za Afya
    Naomba nitoe maoni yangu juu ya Opras: Nashauri mkiona vyema kuwe na opras itakayo kuwa Disignated kwa watumishi wa afya itayopima kazi husika kwa Kada husika. Mfano kuna kuwa na inayowapima Wataalum wa Maabara na kazi zao husika, wauguzi na kazi zao husika. Madaktari ikihusisha Md,Amo,Co,na Aco. Halafu kuwa na za taasisi nyingine kama Elimu, Kilimo na mifugo na nk. Hii itasaidia kutupima vizuri utendaji na kufikia malengo, lakin pia itakuwa rahisi kujua kazi tunazopimwa nazo. Itakua rahisi kujaza kazi husika na kuzifuatilia kwa umakin. Asante.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement