Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema

Serikali imesisitiza maambukizi ya CORONA kweli yapo nchini kwenye baadhi ya mikoa na yanapaswa kuendelea  kudhibitiwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi amesema hayo alipozungumza katika runinga moja hapa nchini.

Ameongeza "Vifo vipo si kwa kiwango kikubwa, hakuna haja ya kuwa na hofu kwani tutaendelea kuishi na COVID -19,  cha muhimu ni kupambana nao Kwa kunzigatia kinga. 

Amesema Serikali kuanzia awamu ya tano iliweza kuamsha mambo mengi baada ya ugonjwa kutokea, na awamu hii ya sita inaendelea na Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuunda  kamati maalumu.

"... na walikuja na ushauri pamoja na mapendekezo 16 ambayo Karibu yote yametekelezwa.

"Mwaka jana nchi iliweza kujiandaa kwa kuandaa miongozo na kutenga maeneo ambayo kama watu watapata maambukizi (isolation center). 

"Wizara tuliandaa miongozo 16 ya kudhibiti CORONA ikiwemo ule wa  elimu, upimaji, kudhibiti misongamano, uvaaji wa barakoa na mwitikio ulikua mkubwa ikiwepo barakoa za kushona wenyewe (barakoa za vitambaa) 

Kunawa mikono pamoja na eneo la tiba asili na dawa za kisasa," amesema.

Ameongeza "Tumesema watu waepuke misongamano hivyo wanaoandaa  shughuli zenye watu wengi na kusababisha  misongamano mikubwa.

“Nashauri... viongozi wa kijamii, wanasiasa na wale wa kidini watafakari vyema kama kweli wana ulazima wa kufanya mikusanyiko mikubwa kwa wakati huu.

Kwa upande wa mipira ya miguu amesema wanashauri kusiwe na watu wengi ili kudhibiti maambukizi, kuvaa barakoa na kunawa mikono kila mara. 

Amesisitiza wananchi wanayo nafasi ya kuhakikisha wanadhibiti ugonjwa huo kama ilivyo mwaka jana.

Ameongeza "Tunaendelea kuhamasisha watu wajikinge kwa sababu huu ugonjwa bado upo hata kama kuna chanjo duniani. 

Amesema wanahimiza wananchi kufanya mazoezi ya mwili na kuzingatia lishe bora ili kuimarisha kinga ya mwili.

"Lazima tuwakinge watu walio kwenye kundi la kuathirika wakiwemo  wenye kisukari, moyo, uzito uliyopitiliza.

"Unawaji wa mikono utasaidia watu wasipate maambukizi, unasaidia pia kuepusha  magonjwa mengine ya mlipuko ikiwemo kipindupindu," ametoa rai. 

Prof. Makubi amebainisha kwamba Serikali imeendelea pia kuimarisha uchunguzi wa hali za afya ya wasafiri katika maeneo ya mipakani

2 Maoni

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement