Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Hatua nne za msingi zimebainishwa Kwa mwananchi anayehitaji kupata chanjo ya CORONA, Tanzania ikiwamo kuwa na kitambulisho kinachotambulika kisheria.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebainisha vituo 550 vya kutolea chanjo hiyo huku ikisisitiza anayehitaji kupata chanjo, kuandaa kitambulisho cha kazi, NIDA, leseni ya udereva, mpiga kura, pasi ya kusafirisha au kingine chochote kinachotambulika kisheria.
 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Abel Makubi amebainisha pia muhusika atatakiwa kujihakiki kama yupo ndani ya makundi matatu ya walengwa kwa sasa.

Ametaja makundi hayo ni watumishi wa sekta ya afya, watu wazima umri wa miaka 50 na kuendelea na watu wenye magonjwa.
Prof. Makubi amesema muhusika atatakiwa kufanya “booking” (miadi) ya siku ya kuchanjwa kwa kutumia mtandao ndani ya simu /Computer(online) yako kupitia https://chanjocovid.moh.go.tz au kwa kwenda moja kwa moja kwenye kituo na kujisajili kuanzia Jumatatu, Agosti 2, 2021 

Amesema pia atapaswa kujaza fomu ya uhiari wa kuchanjwa.

"Wizara inaagiza Waganga Wakuu wa   Mikoa na Wilaya nchini, kukamilisha matayarisho  yote  muhimu  kwa  utoaji  wa  chanjo,  ili  ifikapo  Agosti 03,  2021, utoaji wa chanjo uwe umeanza katika vituo vilivyoainishwa katika mikoa," amesema.

Ameongeza a"Kutokana na uhitaji na mipangilio ya mkoa husika, wanaweza kuongeza idadi ya vituo ili kupunguza msongamano  katika  vituo.  

"Wananchi, watasajiliwa katika mfumo wetu wa Taifa wa Chanjo na watapatiwa cheti baada ya kuchanjwa. 

"Naelekeza pia kwa huu mgao wa COVAX FACILITY ni marufuku Hospitali yoyote (ya umma au binafsi) kulipisha Wananchi gharama yoyotekatika zoezi hili la chanjo na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa wa sasa.  
"Pamoja na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kufanikisha upatikanaji wa chanjo nchini na kuanza kuchanja wananchi, Wizara ya afya inaendelea kuwashauri Wananchi kuendelea kujikinga na UVIKO-19 kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali za mita moja au zaidi, kuepuka misongamano na kufanya mazoezi," amesisitiza. 

Amesema Wizara inamshukuru Rais Samia na serikali ya Marekani, kwa kufanikisha upatikanaji wa chanjo hizo kupitia  mpango wa ugawaji chanjo kwa nchi masikini (COVAX). 

"Pia nawashukuru wadau wetu wote wa chanjo kwa michango yenu mikubwa katika kufanikisha upatikanaji wa chanjo. Serikali inawapongeza sana Viongozi wetu na Wananchi ambao tayari wameitikia zoezi la kuchajwa Kwa hiyari," amesema.

1 Maoni

  1. Nainga mkono zoezi la chajo Ila uangalifu uwepo kuepuka msongamano

    JibuFuta

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement